Tarehe : March 9, 2025, 3:18 p.m.
ILEJE - SONGWE
Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekitii Ndugu Japhet Hasunga walifanya ziara kwenye mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambapo kamati ilitembelea maeneo mbalimbali ya mgodi ikiwemo mradi wa kutengeneza nishati mbadala ya Rafiki Briquette.
Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Deusdedith Magala aliwaongoza wajumbe wa kamati kushudia shughuli mbalimbali zinazofanywa mgodini hapo zikiwemo
Uchimbaji na uchakataji wa makaa ya mawe na mradi wa Rafiki Briquette
Aidha Wajumbe wa Kamati walipongeza mageuzi na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika katika mgodi wa Kiwira .Wajumbe pia waliridhishwa na maendeleo ya mradi wa nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquette na kusisitiza nishati hiyo muhimu iweze kuwafikia wananchi wengi ili kuendelee kuunga mkono ajenda ya upatikanaji wa Nishati safi kwa Watanzania
Aidha mheshimiwa Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa ambae aliambatana na Kamati katika ziara hiyo aliishukuru kamati kwa maoni yao na miongozo mbalimbali wanayoitoka kwa Shirika ambayo imeleta mafanikio makubwa mgodini hapo.
Kabla ya Ziara hiyo ya Kiwira kamati iliweza kupata wasilisho la Utekelezaji wa Shughuli za Shirika tarehe 06.03/2025 Jijini Dodoma katika semina iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Eng Yahya Samamba.
Katika semina hiyo kamati ililipongeza STAMICO kwa mageuzi makubwa yaliyofanywa na Shirika katika kipindi kifupi na kuwataka kuongeza juhudi zaidi ili kuongeza mapato ya Shirika
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.