[Latest Updates]: Jengo Kubwa la Maonesho ya Vito na Mafunzo ya Kuongeza Thamani Madini Kujengwa Arusha

Tarehe : March 13, 2024, 9:57 a.m.
left

-Litagharimu kiasi cha Tsh Bilioni 35

-Kutumika kwenye minada ya madini na mafunzo ya kuongeza thamani madini ya vito

-Kamati ya Bunge yaagiza kuharakishwa kukamilika kwake

-Rais Samia apongezwa kwa mageuzi makubwa sekta ya madini__

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozana na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo imetembelea Kituo cha  Jemolojia Tanzania (TGC) kinachotoa Mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini  kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo  la kituo hicho ambalo litakuwa mahsusi kwa utoaji wa mafunzo ya kuongeza thamani,minada ya madini ya vito na maonesho ya madini.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. David Mathayo amepongeza serikali kwa jitihada za kuboresha mafunzo katika eneo la uongezaji thamani madini ya vito na kutoa maagizo ya uharakishwaji wa taratibu za kuanza ujenzi wa mradi mapema ili manufaa yake kwa watanzania yaonekane.

Akizungumza katika Ziara hiyo Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kwamba jengo hilo pacha(twin tower) lenye thamani ya Tsh Bilioni 35 litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, karakana (viwanda) vya uongezaji thamani madini, maabara za madini ya vito na bidhaa za usonara, mineral gallery, ofisi, mabweni ya wanafunzi, kantini na maduka. 

Mh Mavunde aliongeza pia kwamba Jengo hilo litafungamanisha mafunzo ya uongezaji thamani madini pamoja na viwanda vya uchakataji na biashara ya madini nchini kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo ili kuimarisha umahiri. Mradi huu pia, uhahusisha utolewaji wa mafunzo kwa watumishi kwa lengo la kuwaongezea uwezo (capacity building) pamoja na ununuzi wa vitendea kazi.

 Akitoa taarifa ya Mradi huo Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania(TGC) Mhandisi Ally Maganga ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa ya sekta ya madini na hasa kupitia uongezaji thamani wa madini ya vito ambao utekelezaji wake utachangiwa na kukamilika kwa mradi huu mkubwa na kutumia fursa hiyo pia kuiahidi kamati ya Bunge juu ya usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa mradi  huu kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals