Tarehe : Jan. 17, 2019, 10:45 a.m.
Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameitaka kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya uranium katika mto Mkuju ulioko mkoani Lindi ya Uranium One kutokusita kuwasiliana naye pindi wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa mradi wao.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akisalimiana na Mkurugezni Mkuu wa kampuni ya Uranium One Holdings N.V, Vladimir Hlavinka mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra, Fredrick Kibodya.[/caption]
Aliyasema hayo jana tarehe 15 Januari, 2019 katika kikao chake na watendaji wa kampuni hiyo kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma.
Aidha, Biteko alisema kuwa maombi yote ya leseni kubwa za uchimbaji wa madini zinawasilishwa katika baraza la Mawaziri ili kuweza kuridhiwa baada ya wawekezaji kuonesha nia na kuwasilisha maombi ya leseni hizo.
Biteko alikiri kuwa anao uelewa wa kile kinachoendelea katika uwekezaji huo kutokana na ushirikishwaji alioupata kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki kupitia vikao mbalimbali alivyoshiriki.
Akizungumzia lengo la ujio wao katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uranium One, Frederick Kibodya alisema ni kuelezea maendeleo waliyofikia katika uwekezaji huo pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Madini.
Alisema, uteuzi huo umelenga katika kukuza sekta ya madini ikiwa ni pamoja na mradi wa uchimbaji wa madini ya uranium, “Tunaimani kubwa kwako na tunamshukuru Mungu kwa kukupa nafasi hii” alisema Kibodya.
Akizungumzia uwekezaji uliofanyika mpaka sasa katika mradi huo alisema ni kiasi cha dola za kimarekani Milioni mia mbili ($200mil) kutoka mradi ulipoanza mwaka 2009.
Akizungumzia manufaa ya mradi huo Kibodya alisema ni pamoja na kusaidia katika kukuza teknolojia nchini. Alisema madini hayo yakichimbwa yanatumika katika kuzalisha umeme ambayo ni teknolijia mpya nchini.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra, Fredrick Kibodya akichangia mada katika kikao baina ya wizara na kampuni ya Uranium One Holdings N.V ofisini kwa waziri jijini Dodoma[/caption]
Mradi utasaidia katika kuongeza ajira nchini. Aliendelea kufafanua kuwa kwa kipindi cha ujenzi wa mradi wanatarajia kuajiri watanzania 1600 kwa kipindi cha miezi kumi na nane.
Aidha, alibainisha kuwa kutakuwepo na uzalishaji wa ajila zisiso rasmi kiasi cha watu 4500 wakati wa ujenzi na 2300 pindi uzalishaji utakapoanza.
Alisema, mradi utasaidia katika kuhamisha utaalamu kutoka kwa wawekezaji kwenda kwa wazawa na mradi umelenga katika kutoa elimu ya ajira na utaalamu kwa wazawa.
Pia Kibodya alisema, mradi unatarajia kuliingizia taifa pato la kiasi cha dola za kimarekani milioni 220 kama kodi kwa mwaka, kiasi ambacho kitakuwa kikibadilika kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Mradi wa uchimbaji madini ya uranium katika mto Mkuju unafanywa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Mbia wa kampuni ya Mantra anayejulikana kama Rosatom.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.