Tarehe : Jan. 8, 2019, 10:35 a.m.
Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta,
Waziri wa Madini Doto Biteko amewasili Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kupokelewa na Watumishi wa Wizara ya Madini na baadhi ya Taasisi zake.
Watumishi wa Wizara ya Madini wakimkaribisha Waziri wa Madini Doto Biteko katika wizara hiyo mara baada ya kuwasili kutoka kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Sambamba ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.[/caption]
Biteko aliteuliwa kuwa Waziri wa Madini Januari 8 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa wizara na taasisi.
Akizungumza na watumishi hao, amewataka kujipanga na kushirikiana pamoja na viongozi wa wizara na kuongeza kuwa, wao kama viongozi wanawategemea sana watumishi kuweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
“Mimi sio mgeni ni mwenyeji, wote tunafahamiana. Nawashuru kwa kutupokea mimi na mwenzangu Nyongo. Ninyi ndiyo wenye wizara sisi hatuwezi kuwa hapa kama ninyi hamjatupa ushirikiano,” amesema Biteko.
Ameongeza kuwa, anataka kuona watumishi wa wizara hiyo wakiwa na furaha na kufanya kazi kwa furaha katika kutekeleza wajibu na majukumu ya wizara husika na kueleza kuwa, “Nataka nione wafanyakazi wanafurahi kufanya kazi. Kuna mtu unaweza kumlazimisha kufika kazini lakini si kufanya kazi,” amesema.
Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema mabadiliko yaliyotokea ni kwa ajili ya kuongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya wizara na kuongeza kuwa, Rais Dkt. Magufuli wakati akimwapisha Waziri Biteko Januari 9, alitoa maagizo kwa viongozi hao, ambao wao waliyapokea kwa niaba ya watumishi wote wa wizara na taasisi zake.
Awali, Waziri Biteko alikuwa ni Naibu Waziri katika wizara hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Waziri Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.