Tarehe : Dec. 11, 2024, 7:29 p.m.
BURUNDI YAPONGEZA MAENDELEO SEKTA YA MADINI TANZANIA
Yapongeza maendeleo ya tafiti zilizofanyika
Dodoma
Ujumbe kutoka Burundi ukiongozwa na Mshauri wa masuala ya madini kutoka Wizara ya Madini nchini Burudi wafika Tanzania kujifunza namna bora ya Uongezaji Thamani Madini.
Ujumbe huo umefika leo Desemba 11, 2024 katika Ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Jijini Dodoma na kukutana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt.Mussa Budeba pamoja na wataalamu mbalimbali.
Ujumbe huo ulipokelewa kwa wasilisho maalum kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Huduma za Jiolojia GSS, Yusto Shine kuhusu hatua mbalimbali za maendeleo ya Sekta ya madini hususan katika tafiti zilizofanyika pamoja na ugunduzi wa madini ambayo yanatoa mchango mkubwa kwa taifa na jamii kiuchumi.
Akizungumza kwa niaba ya Ujumbe huo Mshauri wa masuala kutoka Ofisi ya Madini Burundi Niyongabo Regis ameipongeza Sekta ya madini nchini Tanzania kwa maendeleo ya tafiti zilizofanyika nchini ukiwemo utafiti wa Jiofizikia uliofanyika kwa asilimia 16, utafiti wa jiokemia asilima 24 na utafiti wa Jiolojia asilimia 97.
Niyongabo ameeleza kuwa, nchi ya Burundi bado ipo katika hatua mbalimbali za kuendeleza Sekta ya Madini na Nishati katika kuunganisha kwenye mnyororo wa thamani kuanzia ngazi ya utafiti, uzalishaji mpaka katika masoko ya ndani na nje ya Burundi.
Niyongabo ameongeza kuwa kupitia Makubaliano ya Mashirikiano ya Kikazi (MoU), ambapo malengo ya Burundi ni kupiga hatua kama ilivyo Tanzania kwasababu inaaminika kuwa Maendeleo ni hatua na michakato ya mageuzi.
Awali, akiukaribisha ugeni, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kitaalam ambao utahusisha hatua zote za jiosayansi ikiwemo uchakataji wa taarifa za ugani wa jiolojia, jiokemia, jiofizikia na uchapishaji wa ramani.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.