[Latest Updates]: Tutatoa Leseni ya Madini kwa Yeyote-Biteko

Tarehe : Feb. 6, 2020, 8:52 a.m.
left

Na Issa Mtuwa – Dodoma

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema utaratibu wa upatikanaji wa leseni za madini za aina mbalimbali hupatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu. Amesema, sheria hizo hutumika kulinda leseni hizo ili ziwe hai. Kwa kuzingatia masherti yaliyomo kwenye leseni, atakayeshindwa kuzingatia masherti hayo sheria hutumika ikiwemo kutoa hati ya makosa (default notes) na hatimae kuzifuta.

Biteko ameyasema hayo leo tarehe 6/02/2020 wakati wa kikao chake na kampuni ya Peak Resources Ngwala (PRNG) ofisini kwake jijini Dodoma akizungumzia masuala ya utoaji wa leseni za uchimbaji madini. PRNG walikuwa wakifuatilia upatikanaji wa leseni ya uchimbaji madini ambapo Biteko amesema suala lao linashugulikiwa na taratibu zikikamilika watapatiwa.

Amesema wakati wa sasa suala la leseni siyo kificho na halihitaji kumuona mtu ili upate leseni, kubwa ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuzingatia sheria. Ameongeza kuwa leseni ya PRNG ikikamilika itatolewa.

Mkurugenzi wa PRNG Luca Stanfield amemshukuru waziri kwa mazungumzo yake huku wakisema wanachosubiri kupata leseni ili waanze kazi na watafwata sheria.

Biteko amesema leseni zinatolewa kwa kila mtu iwe wa ndani au nje ya nchi anapaswa kuzingatia sheria na taratibu. “Kwenye utoaji wa leseni kuna sheria za kuzingatia ikiwemo ulipaji tozo za kodi za serikali ambazo muombaji anapaswa kuzifahamu na kulipa” amesema Biteko.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals