[Latest Updates]: Madini Waainisha Fursa kwa Wawekezaji Kutoka India

Tarehe : July 14, 2023, 10:30 a.m.
left

Sekta ya Madini imekuwa miongoni mwa Sekta zilizopata nafasi ya kunadi fursa zake za uwekezaji kwa ujumbe wa  Wawekezaji kutoka Jimbo la Haryana nchini India.

Ujumbe huo wa wawekezaji takribani 150 unashiriki  katika  Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara SabaSaba yanayoendelea jijini Dar Es Salaam.

Akitoa wasilisho kuhusu Sekta ya Madini nchini na fursa zilizopo, Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Madini Veronica Nangale ameelezea fursa ambazo wawekezaji hao wanaweza kushirikiana na Tanzania kuwa ni pamoja na  utafiti wa madini, uchimbaji, biashara ya madini, uongezaji thamani madini na miradi ya ubia kupitia Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) na kampuni nyingine za ndani.
 
Veronica ameeleza kuhusu utajiri ambao  nchi ya Tanzania  imebarikiwa kuwa nao na kuongeza kwamba, zipo fursa nyingi katika sekta ya madini ambayo nchi hiyo inaweza kuzitumia suala ambalo litaongeza ushirikiano ambao nchi hizo mbili zimekua nao kwa miaka mingi.

Baada ya wasilisho hilo na mengine, wawekezaji hao wamepata nafasi ya kukutana ana kwa ana na wataalam wa  sekta zilizotoa  mada ili kupata taarifa zaidi za kina na kukaribishwa kutembelea banda la madini kukutana na wadau wengine wanaoshiriki maonesho katika banda hilo.

Wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza katika  madini ya phosphate, quarz, colbat, lithium, mawe ya nakshi na baadhi wakitaka kupata taarifa zaidi kuhusu miradi ya ubia.

Sekta nyingine zilizotoa wasilisho katika Siku hiyo ya India ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  Wakala wa Misitu Tanzania(TFS), EPZA na  ZPA.

Jukwaa hilo limelenga kujenga mahusiano na ushirikiano wa kibishara, kiuwekezaji kati ya Tanzania na India.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals