[Latest Updates]: Utekelezaji MoU Tanzania na Burundi Waanza Rasmi

Tarehe : Dec. 12, 2024, 7:38 p.m.
left

Ni kubadilishana uzoefu katika Utafiti wa kina katika madini

Ni wa Uongezaji thamani madini

Na Usimamizi wa Sheria na taratibu za biashara ya madini

Dodoma

Itakumbukwa kwamba mwezi machi 30, 2024 jijini Bujumbura nchini Burundi, Waziri wa Madini Tanzania Mhe. Anthony Mavunde na Waziri wa Maji, Nishati na Madini nchini Burundi Mhandisi Ibrahim Uwizeye kwa pamoja walisaini Hati ya Makubaliano (MoU) kuhusu  Ushirikiano wa kikazi katika Sekta ya Madini kupitia mikakati mbalimbali ya kisekta ili kuendeleza uchumi wa nchi zote mbili.

Katika kutekeleza mashirikiano hayo , mnamo Desemba 11, 2024 Ujumbe maalum kutoka Serikali ya  Burundi ulifika Tanzania na kukutana na uongozi na wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ukiwa na lengo la kujifunza kuhusu maendeleo ya Sekta ya Madini katika mnyororo wa thamani madini hususan katika vipengere vya Uongezaji thamani madini, tafiti za kina , namna bora ya kusimamia Sheria na taratibu za biashara ya madini.

Kwa mujibu wa MoU, Tanzani ikiwa na uzoefu wa muda mrefu katika Sekta ya Madini itatoa Utalaam wake nchi ya Burundi katika  kuimarisha taratibu za uchimbaji salama  na endelevu.

Aidha, itatoa mafunzo na kugawana maarifa kuhusu teknolojia ya kisasa na kuanzisha miradi ya pamoja  ya utafiti  wa madini ambapo  kwasasa Burundi inatafuta kuboresha miundombinu na teknolojia ya uchimbaji.

Sambamba na hapo, pande zote mbili zitajadiliana kuhusu ujenzi wa viwanda vya uchakataji, uchenjuaji na usafishaji madini pamoja na kujengeana uwezo kwa taasisi na wataalam wa pande zote.

Ujumbe huo umeongozwa na Niyongabo Regis ambaye ni mshauri wa masuala ya  madini kutoka Wizara ya Maji , Nishati na madini nchini Burundi.

Pamoja na mambo mengine , ujumbe huo utapata fursa ya kujifunza hatua za maendeleo ya sekta  ya madini kupitia taasisi tendaji  zilizochini ya Wizara ya Madini ambazo ni taasisi ya GST, STAMICO,Tume ya Madini,TEIT na TGC.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals