[Latest Updates]: Serikali Yaongeza Umiliki wa Hisa Mgodi wa Mwadui- Waziri Mavunde

Tarehe : Nov. 7, 2023, 9:05 a.m.
left

# Asema imefikisha asilimia 37

# Kiasi cha Shilingi bilioni 41.6 kinatarajiwa kutumika katika kulipa fidia mgodi wa kabanga Nikeli

Kutokana na Mabadiliko ya Sheria ya Mwaka 2017 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeongeza umiliki wa hisa katika Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Almasi ijulikanayo kama Williamson Diamonds Limited na kufikia asilimia 37 tofauti na awali ilikuwa na asilimia 25.

Kupitia mabadiliko hayo Serikali imeweza kusaini mikataba ya ubia na kuunda kampuni tano za ubia kwa ajili ya uchimbaji madini Wa kati na uchimbaji mkubwa , kampuni hizo ni pamoja na Tembo Nickel Corporation Ltd, Sotta Mining Corporation Ltd, Faru Graphite Corporation Ltd, Duma TanzGraphite Ltd na Mamba Minerals Corporation Ltd.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu uendelezaji wa leseni za madini , Mhe.Waziri Mavunde alisema kuwa tarehe 19 Januari 2021 Serikali kupitia kampuni ya Tembo Nikeli (TNCL) iliingia ubia wa umiliki wa asilimia 16 na Kampuni ya _LZ Nickel_ ya Uingereza yenye hisa asilimia 84 kwa mradi wa uchimbaji madini ya Nikeli katika mkoa wa Kagera wilayani Ngara.

Akielezea maendeleo ya mradi huo Mhe.Mavunde alieleza kuwa uzalishaji wa mbale ya Nikeli pamoja na madini ambata unatarajiwa kuanza mwaka 2026 baada ya kukamilisha hatua za ulipaji wa fidia kwa wananchi na kuanza usimikaji wa mitambo.

Aidha, aliongeza kuwa mpaka kufikia mwezi Oktoba 2023 , kampuni ya TNCL ilikuwa imekamilisha uthaminishaji wa wananchi 1,341 na kuweza kulipa kiasi cha Shilingi za kitanzani bilioni 33.08 kama fidia kwa wananchi wakaopisha mradi katika vijiji vya Bugarama , Rwinyana , Nyabihanga , Mukubu, Mumiramira na Muganza ambapo mpaka kukamilika kiasi cha Shilingi bilioni 41.6 za kitanzania zinatarajiwa kutumika.

Mradi wa uchimbaji madini ya Nikeli una maeneo mawili ambapo eneo la kwanza lina hekta zaidi ya 4,000 zimetengwa kwa ajili ya uchimbaji mkubwa wa madini ya Nikeli wilayani Ngara eneo la Kabanga, ambapo uchimbaji mkubwa utafanyika kwa kipindi cha takribani miaka 33.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals