[Latest Updates]: Burundi na Tanzania Zasaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano Kwenye Sekta ya Madini

Tarehe : March 30, 2024, 8:09 a.m.
left

Bujumbura,Burundi.

Mawaziri wa Sekta ya Madini wa Burundi Mh. Eng. Ibrahim Uwizeye na Tanzania Mh. Anthony Mavunde leo wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kwenye sekta ya madini ili kukuza mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi mbili hizi.

Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo Jijini Bujumbura,Burundi na kuhudhuriwa na watalaamu wa nchi zote mbili.

Maeneo ya Ushirikiano yanajumuisha;

- Ujenzi wa Viwanda vya Uchenjuaji na Usafishaji wa Madini.
- ⁠Kubadilishana Uzoefu na utaalamu katika utafiti wa kina wa madini.

- ⁠Kuongeza thamani ya madini kwa kuzalisha bidhaa zitokanazo na madini.

- ⁠Kujenga uwezo wa kitaasisi na wataalamu wa pande zote mbili.

- ⁠Kusimamia sheria na taratibu za biashara ya madini inayohusisha pande zote mbili.

Akitoa maelezo ya awali Waziri wa Maji,Nishati na Madini wa Jamhuri ya Burundi Mh. Eng. Ibrahim Uwizeye amesema nchi ya Burundi
na Tanzania zimekuwa na urafiki wa muda mrefu na mahusiano mazuri,hivyo ni muhimu kutumia fursa hii kushirikiana kwenye sekta ya madini ili sekta hii itoe mchango unaostahili katika kukuza maendeleo ya Uchumi wa Burundi na Tanzania chini ya uongozi imara wa marais Mh. Evariste Ndayishimiye(Burundi) na Mh. Dkt. Samia S. Hassan (Tanzania)

Akizungumza katika hafla hiyo ,Waziri wa Madini wa Tanzania Mh. Anthony Mavunde amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na Burundi katika kuiimairisha na kuiboresha sekta ya madini ya nchi hizi mbili kwa kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa na kutumia fursa hii kuwaalika wachimbaji wa nickel,cobalt na copper kutumia huduma ya Kiwanda cha Usafishaji madini ambacho kitajengwa katika eneo la ulipokuwa Mgodi wa Buzwagi,Wilayani Kahama-Shinyanga.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals