[Latest Updates]: Mradi Mkubwa wa Uchimbaji Madini Tembo Tanzania Kuzalisha Malighafi za Injini za Ndege, Nyuklia, na Vifaa Tibae

Tarehe : Feb. 20, 2024, 10:17 p.m.
left

Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuwezesha upatikanaji wa Leseni Kubwa ya uchimbaji madini (Special Mining License - SML) kwa Kampuni ya Nyati Mineral Sands inayomilikiwa  kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Strandline ambayo itapelekea kuanza kwa mradi mkubwa wa uchimbaji Madini Tembo katika Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.

Hayo yameelezwa leo tarehe 20 Februari na, 2024 na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde alipofanya ziara ya kutembelea sehemu ya eneo la mradi huo iliyopo katika kijiji cha Stahabu, Kata ya Mikinguni Wilayani Pangani-Tanga.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wizara ya Madini kuhakikisha tunawezesha uanzishwaji wa miradi hii mikubwa na ya kimkakati ambayo itapelekea si tu ustawi wa uchumi wa Nchi yetu, bali kuwa kichocheo cha maendeleo na ustawi wa Wilaya ya Pangani na wananchi wanaozunguka mradi huu.

Amesema ni dhamira ya Serikali  kuona wawekezaji wakubwa wenye nia njema na nchi ya Tanzania  wanapewa ushirikiano ili kuwezesha shughuli zao kwa manufaa ya Taifa. 

Mradi huo unatarajiwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 125 ambao uhai wake unakadiriwa kuishi kwa miaka 20 hadi 25 utatekelezwa katika Vijiji 8 vilivyopo katika Kata za Mikinguni, Mwera, Tungamaa na Bweni-Wilaya ya Handeni,Mkoani Tanga.

"Nimefurahishwa na utayari wa wananchi wanaoguswa na mradi kupisha kuanza kwa mradi, na kwa kuwa ni hatua muhimu sana kwani itarahisisha kuanza mradi kwa wakati na kuondoa changamoto ya migogoro kati ya wananchi na mwekezaji," amesema Mavunde.

Akizungumza kwa niaba ya Mwekezaji, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyati Mineral Sands Ltd ambaye anawakilisha Hisa za Serikali, Mhandisi Heri Gombera amesa kwamba mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka 2026 na unatarajiwa kuzalisha tani milioni 8 za madini mbalimbali  kwa mwaka yakiwemo titanium, ilmenite, rutile, zircon na monazite ambayo pamoja na matumizi mengine hutumika pia kuzalisha malighafi za injini za ndege, nyuklia,vifaa vya hospitali na viwanda vya marumaru na rangi.

Aidha, Mhandisi Gombera amebainisha kwamba Kampuni ya Nyati Minerals Sand ipo tayari kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo na kuongeza kuwa pindi watakapopata Leseni yao kwa kushirikiana na Wadau wote wataanza zoezi la tathmini na ulipaji wa fidia kwa wananchi ili kupisha kuanza kwa mradi huo.
 
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Zainab Abdallah amemahukuru Mhe Rais Samia  kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini ambayo yamepelekea mradi huo  kuanzishwa Wilayani Pangani na  kwamba pindi mradi huo utakapoanza utaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Pangani kuongeza kipato chao na kujikimu kutokana na ujira watakaokuwa wanaupata kutoka kwenye mradi sambamba na kuchochea uchumi wa  wilaya hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals