[Latest Updates]: Mavunde Aitaka TEITI Kuwa Kitovu cha Taarifa za Madini

Tarehe : Sept. 12, 2023, 11:36 a.m.
left

Ataka Taarifa za TEITI zisaidie kuongeza mapato

TGC kufanyia kazi waliyojifunza China,Thailand

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameitaka Taasisi ya Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini (TEITI) kuwa kitovu cha taarifa za rasilimali madini ili kuisadia serikali na Wizara katika ukusanyaji wa mapato kutoka katika rasilimali za hiyo ili kuongeza tija  katika mnyororo mzima wa sekta ya madini nchini. 
 
Waziri Mavunde ametoa  maelekezo  hayo leo septemba 12, 2023 wakati akizungumza katika kikao na  TEITI pamoja na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Mhe . Mavunde amesema TEITI ina jukumu kubwa la kukusanya taarifa na takwimu zinahusu rasilimali madini  hivyo ni matarajio kuwa taarifa au takwimu hizo zitasaidia Wizara katika mipango yake ya kuongeza mapato.

“Sekta hii ni kubwa sana, ili kufikia lengo la kuongeza mapato ya serikali tunapaswa kuwa na taarifa sahihi zilizofanyiwa utafiti pamoja na takwimu sahihi za mapato ambazo zitaiongoza wizara kujua ni eneo gani linapaswa kuongezewa nguvu zaidi hii ni kutokana na  TEITI yenyewe kuwa  ni kitovu cha taarifa zote zinazohusu rasilimali madini" amesema Mavunde. 

Akizungumzia  kuhusu TGC, Waziri Mavunde amekitaka kituo hicho kusaidia Wizara kufikia lengo la kuongeza thamani madini ili kutimiza lengo la kuanzishwa pamoja kuyafanyia kazi yale mliyojifunza katika ziara ya China na Thailand

“Nimesikia kuwa mlitembelea nchi ya China na Thailand, ni matumaini yangu kuwa mtayafanyia kazi  yale mliyojifunza huko, ujuzi huo mlioupata huko tuone ukipatikana hapa ndani ya nchi na tuwajengee uwezo watu wetu ili wafanye vizuri zaidi katika eneo hilo la kuongeza thamani madini yetu” amesema Mavunde. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema lengo la kuanzishwa kwa TEITI ni kuhakikisha wizara inakuwa na Takwimu sahihi zinazohusu rasilimali Madini ili zisadie  katika kufikia malengo yake yakiwemo ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. 

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya amesema kuwa TEITI imepanga kuweka wazi mikataba ya serikali na makampuni yaliyowekeza katika rasilimali zao ili kuweka uwazi wa mikataba hiyo.

Ameongeza kuwa TEITI inatarajia kuweka wazi kiasi cha hisa za serikali kwa kampuni zinazoingia nayo ubia hapa nchini ili wananchi wafahamu mawanda ya umiliki wa hisa ya serikali katika kampuni hizo na manufaa yanayopatikana.

Pia,  ameeleza kuwa TEITI imepanga kufanya Tafiti kwenye shughuli za sekta ya madini ili kuweka wazi kuhusu uharibifu wa  mazingira sambamba na mchango wa wachimbaji wadogo katika sekta ya madini ambao kwa siku za karibuni umeongezeka sana.
 
 Akizungumza Kwa niaba ya Mratibu wa TGC, Kaimu Mratibu Msaidizi, Kurugenzi ya Mipango, Tafiti na Uendelezaji Ujuzi wa kituo hicho, Jumanne Shimba amesema kuwa kituo hicho kimepanga kuwa na maabara yenye viwango vya kimataifa ili kutoa huduma za uongezaji thamani madini kwa viwango vya kisasa

Pia amesema kuwa Kituo hicho kimepanga kuanzisha vituo ambayo vitatangaza fursa ya Madini nchini ambapo tayari wameshaanza katika baadhi ya viwanja vya ndege ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals