[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yatoa Kongole Maonesho ya Geita

Tarehe : Sept. 19, 2020, 10:57 a.m.
left

Steven Nyamiti na Tito Mselem

Viongozi  na Wataalam wa Wizara ya Madini wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo ndani ya viwanja vya Maonesho hayo.

Mhandisi Gabriel amewaeleza Wataalam na Viongozi wa Wizara ya Madini namna Mkoa wa Geita unavyosimamia shughuli za uchimbaji madini kwa ushirikiano na Afisa Madini Mkoa.

Mhandisi Gabriel amewataka Wadau kushirikiana na Wizara hususani Wachimbaji Wadogo ili kuchimba kwa tija kwa kutumia Teknolojia rahisi na za kisasa.

Wakati huo huo, Viongozi hao wametembelea banda la Wizara ya Madini na kupongeza maandalizi mazuri yaliyofanyika na namna wanavyo elimisha umma juu ya masuala mbalimbali yanayosimamiwa kwenye Sekta ya Madini ikiwepo Sheria na Kanuni mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini, Dkt. Mussa Budeba amewapongeza waandaaji wa banda la Wizara ya Madini kwa kuonesha ushirikiano mkubwa katika kutoa elimu kwa Wachimbaji Wadogo katika maonesho hayo.

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel, Kamishina Msaidizi wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wazawa katika Uchumi wa Madini (Local Content) Terrence Ngole, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa uratibu mzuri wa maonesho hayo.

Maonesho hayo yenye Kauli mbiu “Madini ni Uchumi,  2020 Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Taifa”   yanahudhuliwa na Kampuni zaidi ya 420.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals