Tarehe : Jan. 7, 2019, 10:32 a.m.
Na Asteria Muhozya,
Watumishi wa Wizara ya Madini wameungana na watumishi wengine nchini kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutangaza kutumika kwa kikokotoo cha zamani cha mafao ya Wastaafu.
Wafanyakazi wa Madini wakishiriki maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania uamuzi wake wa kutangaza kutumika kwa kikokotoo cha zamani cha mafao ya Wastaafu.[/caption]
Watumishi hao wameungana katika maandamano ya amani yaliyoanzia katika Ofisi za Bunge na kupokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika Bustani za Nyerere Square, jijini Dodoma.
Akizungumza na watumishi kutoka sekta mbalimbali, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi katika hatua zote za majadiliano ya suala hilo hadi pale pande zote zitakaporidhika.
Ameongeza kuwa, maombi yaliyowasilishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) yameanza kufanyiwa kazi na mengine yanaendelea kufanyiwa kazi.
Akizungumzia ombi la mishahara mipya ya wafanyakazi amesema Tume ya Mishahara na Motisha inaendelea kulifanyia kazi suala hilo na pindi litakapokamilika, taarifa itatolewa.
Kuhusu madeni ya watumishi amesema serikali inaendelea kulipa madeni hayo ikiwemo malimbikizo mbalimbali ya watumishi.
Kuhusu kupandishwa madaraja, amesema tayari Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza kushughulikia suala hilo ambapo tayari utekelezaji umekwisha anza kwa baadhi ya sekta na kuongeza kwamba serikali itaharakisha suala hilo ili wenye sifa wapate madaraja mapya.
Aidha, amesisitiza kwamba serikali iko pamoja na watumishi wote na haitowaangusha na kuwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi.
Wafanyakazi wa Madini wakishiriki maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania uamuzi wake wa kutangaza kutumika kwa kikokotoo cha zamani cha mafao ya Wastaafu.[/caption]
" Tuendelee kujituma. Kazi zinazofanyika zinaonekana. Hata utoaji huduma unaendelea vizuri. Uko umoja wa wafanyakazi unaonekana na watumishi wanawahudumia wananchi," amesema Waziri Mkuu.
Katika hatua nyingine ameendelea kusisitiza suala la kutowahamisha watumishi bila kulipwa fedha za uhamisho.
Awali, akisoma hotuba ya Wafanyakazi, Katibu Mkuu wa TUCTA amemweleza Waziri Mkuu kuwa bado kiwango cha mishahara wanayolipwa watumishi hakitoshi na kuongeza kuwa bado wafanyakazi wanabeba mzigo wa kodi ya mapato hususan wale wenye viwango vya juu vya madaraja.
Aidha, amemweleza Waziri Mkuu kuwa viongozi waache kunyanyasa wafanyakazi na pindi wanapoondolewa kwenye utumishi waondolewe taratibu za kazi.
Mwisho ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa matumizi ya mifuko hiyo.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.