[Latest Updates]: Kamati ya Bunge Nishati na Madini Kujifunza Uongezaji Thamani Madini Zambia

Tarehe : Jan. 13, 2025, 1:32 p.m.
left

Zambia

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiongozwa na Mbunge wa Geita Mjini anayemwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu wako nchini Zambia katika ziara ya mafunzo kuhusu Uongezaji Thamani Madini.

Mhe. Kanyasu ameambatana na wajumbe wengine watatu wa Kamati hiyo akiwemo Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mhe. Aleksia Kamguna na Mhe. Janeth Mahawanga pamoja na Katibu wa Kamati, Bw. Chacha Nyakenga. Kwa upande wa Wizara, ujumbe huo unawakilishwa na Kamishna Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani Madini Bw. Archard Kalugendo.

Ziara hiyo, iliyoandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, ilianza Januari 12 na inalenga kuwapatia uelewa wabunge hao katika masuala ya uongezaji thamani madini na ushirikishwaji wa jamii nchini humo na inatarajiwa kukamilika Januari 16, 2025.

Leo tarehe Januari 13 2025, ujumbe huo ukiambatana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt. Gen. Matthew Mkingule, umetembelea Wizara ya Migodi na Maendeleo ya Madini, nchini humo ambapo wamekutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hapenga Kabeta na maafisa mbalimbali wa Wizara hiyo. Aidha, ujumbe huo umetembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia na kukutana na maafisa Ubalozi. 
#ValueAdditionforSocio-EconomicDevelopment

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals