Tarehe : June 14, 2018, 11:42 a.m.
Balozi wa Australia nchini Tanzania, Alison Chartres, amemtembelea Waziri wa Madini Angellah Kairuki na kuzungumzia ushirikiano wa nchi hizo katika sekta ya madini.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati-waliokaa), Balozi wa Australia nchini Tanzania, Alison Chartres (kushoto-waliokaa) na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kulia-waliokaa); wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Kampuni za Madini na Nishati za Australia na wataalam wa sekta ya madini Tanzania, baada ya kikao baina ya pande hizo mbili kujadili ushirikiano katika sekta ya madini. Kikao kilifanyika Juni 13, 2018 Makao Makuu ya Wizara Dodoma.
Akiongoza Ujumbe wa Umoja wa Kampuni za Madini na Nishati za Australia, Juni 13, 2018 Makao Makuu ya Wizara Dodoma; Balozi Chartres alimweleza Waziri Kairuki kuwa nchi yake inapenda kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya madini.
Kwa upande wake, Waziri Kairuki; pamoja na kumhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kadri inavyotakiwa kwa Australia, lakini pia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali wa nchi hiyo, waendelee kuja kuwekeza katika sekta ya madini nchini na katika sekta nyingine pia.
“Ni matumaini yetu kuwa, nchi zetu zitaendeleza ushirikiano katika sekta ya madini na sekta nyingine mbalimbali kama ambavyo tumekuwa tukifanya,” alisisitiza Waziri.
Aidha, Waziri Kairuki aliuelekeza Ujumbe huo kutoka Australia, kuwasilisha mapendekezo rasmi kwa Serikali ikiwa kuna eneo lolote katika sekta ya madini, wanalodhani linahitaji kufanyiwa marekebisho ili wataalam wayapitie na kuona endapo yana tija kwa pande zote mbili, na kisha kufikia maamuzi.
“Niweke wazi kuwa, Serikali ya Tanzania imedhamiria kuhakikisha kuwa sekta ya madini inawanufaisha wananchi wake ipasavyo. Kwa hiyo, kila tutakapobaini kuwa liko eneo ambalo halituridhishi, hatutasita kufanya marekebisho kwa manufaa ya Watanzania wote.”
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi David Mulabwa pamoja na maafisa mbalimbali waandamizi kutoka Wizara ya Madini na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Imeandaliwa na:
Veronica Simba, Dodoma
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
Kikuyu Avenue,
P.O Box 422,
40474 Dodoma,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
BaruaPepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.