[Latest Updates]: Mbibo Apongeza Mchango wa Wajiolojia/Wanajiosayansi Matumizi Nishati Safi

Tarehe : Dec. 4, 2024, 10:42 a.m.
left

Awataka kuwa watulivu suala la Bodi ya Usajili wa wanajiosayansi likifanyiwa kazi

Tanga

Serikali imepongeza mchango wa Wajiolojia na Wajiosayansi katika kusaidia kuhama kutoka matumizi ya nishati chafu kwenda nishati safi ikiwemo azma ya kutumia utajiri wa madini ya Tanzania kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi.

Hayo yamebanishwa leo Desemba 4, 2024 jijini Tanga na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini  Msafiri Mbibo kwa niaba ya  Waziri wa Madini wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wajiolojia  nchini.

‘’Ni ukweli usiopingika kuwa rasilimali madini zilizogunduliwa Tanzania, rasilimali ya gesi asilia, gesi ya helium na rasilimali zingine ni matokeo ya utaalamu wa wanajiosayansi. Kwa hili tunawapongeza sana,’’ amesema Mbibo.

Ameongeza kwamba, Serikali imeendelea kutumia wanajiosayansi katika kufanya tafiti kwa lengo la kubaini uwepo wa madini nchini kupitia maono ya Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri na kueleza kwamba katika kufanikisha maono hayo, wanajiosayansi wameendelea kutumia utaalamu wao katika kufanya utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa lengo la kutambua tabia za miamba.

Ameeleza kwamba, Sekta ya Madini nchini imeendelea  kuimarika na kufanya vizuri mwaka hadi mwaka huku ikiendelea kuchangia katika uchumi na mapato ya Serikali ikiwemo ongezeko la ajira za moja kwa moja kwa Watanzania ambapo zimefikia zaidi ya 16,000, huku nafasi za juu kwa baadhi ya miradi mikubwa zikiwa mikononi mwa watanzania.

Pia, Mbibo ameeleza kuhusu hatua mbalimbali za kimkakati zilizochukuliwa na Serikali zenye lengo la kuimarisha sekta ya madini nchini na kuzitaja baadhi kuwa ni pamoja na  kuanzishwa kwa masoko na vituo vya ununuzi wa madini nchini; utekelezaji wa ajenda ya kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi badala ya kusafirisha madini ghafi;

Amezitaja hatua nyingine kuwa ni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya wachimbaji wadogo; utekelezaji wa programu mbalimbali za kama vile Mining for Brighter Tomorrow (MBT); na usimamizi makini wa utekelezaji wa Kanuni za Maudhui ya Ndani yaani Local Content.  

Akizungumzia changamoto ya muda mrefu ya kutokuwepo kwa Bodi ya Usajili wa wanajiosayansi, inayoikabili Jumuiya ya Wanajiosayansi nchini, Mbibo amewataka kuendelea kuwa watulivu wakati Wizara kushirikiana na Uongozi wa Jumuiya wa Wajiolojia Tanzania inaendelea kulifanyia kazi suala hili.

Mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘’kutumia utajiri wa madini ya Tanzania kwa mendeleo endelevu ya kiuchumi na kuhama kutoka matumizi ya nishati chafu kwenda nishati safi’’.

#Vision2030:MadininiMaishanaUtajiri
 UongezajiThamaniMadinikwaMaendeleoyaKiuchuminaKijamii

#InvestINTanzaniaMiningSector

#ValueAdditionforSocioEconomicDevelopment

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals