[Latest Updates]: Dkt. Mpango Ailekeza Wizara ya Madini Kusimamia Madini Mkakati kwa Manufaa ya Watanzania

Tarehe : Aug. 23, 2024, 12:13 a.m.
left

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Madini kuhakisha inasimamia vyema uvunaji wa madini ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika nayo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Katika eneo la Mpwayungu, Wilaya ya Chamwino-Dodoma wakati akihitimisha ziara ya siku 4 ya Mkoa wa Dodoma.

“Mwenyezi Mungu ametujaalia rasilimali hii ya madini mkakati yenye mahitaji makubwa sana Duniani," amesema Dkt. Mpango.

Amesema Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini  mkakati kwa wingi na aina tofauti tofauti, na kueleza kuwa ni  lazima rasilimali  hiyo ikatafsirike katika maendeleo ya wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

"Wizara ya Madini hakikisheni mnaweka mpango mzuri wa usimamizi wa rasilimali hii kwa manufaa ya Taifa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo” amesema Dkt. Mpango.

Akiwasilisha salamu za Wizara Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde amemwahidi Dkt.Mpango kuyafanyia kazi maelekezo yote na kwasasa Wizara inakamilisha andiko la mkakati wa usimamizi na uvunaji wa madini hayo ili yalete faida kwa nchi kwa  kuchochea uchumi na kuendeleza sekta ya madini.

Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Maafisa Madini Wakazi kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maeneo yenye uchimbaji wa madini mkakati ili manufaa yake yaonekane kwa Taifa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals