[Latest Updates]: GST na BGS Zafanya Majadiliano Namna ya Kuanzisha Mashirikiano Katika Tafiti na Kujengeana Uwezo

Tarehe : Dec. 12, 2024, 7:40 p.m.
left

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Jiolojia ya nchini Uingereza (BGS) zimefanya mazungumzo ya namna bora ya kuanzisha mashirikiano katika tafiti za madini na kujengeana uwezo. 

Taasisi hiyo ya Jiolojia kutoka nchini Uingereza ikuwa na GST kwa muda wa siku 3 kwa lengo la kujifunzo namna GST inavyotekeleza majukumu yake kwa kufanya ziara ya kujifunza katika Kurugenzi ya Huduma za Jiolojia, Kanzidata na Maabara. 

Akizungumza wakati wa kuhitimisha, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amewashukuru wataalamu hao kutoka BGS kwa kuona umuhimu wa kuanzisha mashirikiano na GST na kuahidi kutoa ushirikiano katika kufikia lengo lililokusudiwa.

Amefafanua kuwa, ushirikiano huo umelenga katika matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kutafiti madini ya kimkakati,  kuratibu majanga ya asili ya jiolojia pamoja na kujengeana uwezo kwa kubadilishana uzoefu. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Budeba amewazawadia watalaamu hao wa BGS toleo jipya la kitabu cha madini viwanda kama sehemu ya kuvutia uwekezaji mkubwa katika madini viwanda ambapo miongoni mwao yamo madini ya kimkakati.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals