[Latest Updates]: Waziri Mavunde Asisitiza Kipaumbele cha Serikali Katika Uongezaji Thamani Madini

Tarehe : May 17, 2024, 10:14 p.m.
left

● Akaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya kuzalisha bidhaa zitokanazo na madini

● Viwanda vya kuzalisha malighafi ya betri za magari ya umeme kujengwa Kahama,Shinyanga


Katika kuhakikisha rasilimali madini ambazo  nchi ya Tanzania imejaliwa na Mwenyezi Mungu zinawanufaisha watanzania , Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha madini yote yanaongezwa thamani hapa nchini kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Hayo yalibainishwa  Mei 16,  2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam  aliposhiriki hafla ya kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya PULA Group.

"Mhe Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuagiza sisi wasaidizi wake kuhakikisha tunasimamia uongezaji thamani wa rasilimali madini ili yanufaishe watanzania wengi zaidi ndiyo  sababu  tunasimama kifua mbele kutekeleza maagizo hayo ya Serikali kwa maslahi mapana ya Nchi yetu" alisema Mavunde.

Aliongeza kuwa, ni dhamira  ya Serikali kuona kwamba madini yote yanasafirishwa yakiwa yameongezwa thamani sababu ambayo imepelekea  Wizara kuweka mkakati ambao pamoja na kuvutia uwekezaji, umeweka sharti la uwekezaji huo uendane samamba na uongezaji thamani wa madini yatakayochimbwa.

Vilevile, Mhe Mavunde alitoa rai kwa wawekezaji wengi kuchamgamkia fursa ya uwekezaji kutokana na  nchi ya Tanzania kubarikiwa  madini ya aina nyingi, ikiwemo mazingira mazuri ya uwekezaji na miundombinu ya kisasa ambayo yanarahisisha uwekezaji wa aina yeyote katika sekta ya madini.

Akisisitiza kuhusu  nafasi ya Tanzania katika mwelekeo wa dunia kwenye Nishati safi, Waziri Mavunde alieleza kuwa kama nchi ipo tayari kupokea wawekezaji katika madini mkakati na muhimu ambayo  imejiwekea utaratibu ambao utawezesha kuyaongeza thamani hapa nchini kabla hayajasafirishwa nje ya nchi.

"Ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita kwenye sekta ya madini ambapo, tunahitaji betri za kufungwa kwenye magari ya umeme zitengenezwe hapa nchini Tanzania na kupelekwa kufungwa kwenye magari moja kwa moja popote pale duniani", alibainisha Mhe. Mavunde.

Awali, akitoa salamu za ubalozi, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Michael  Battle alieleza kuwa dunia kwa sasa imeweka kipaumbele katika nishati safi, ambayo inatokana na madini muhimu na mkakati, na hivyo  kutoa wito kwa Tanzania kuwalazimisha na kuwaomba wawekezaji wote watakaofika kwenye sekta ya madini sharti waongeze thamani hapa hapa nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampuni ya PULA, Balozi Charles Stith alibainisha kwamba hakujiuliza mara mbili kuleta uwekezaji nchini Tanzania kutokana na kama nchi kubarikiwa uongozi thabiti na imara unaovutia na kulinda maslahi ya wawekezaji na kuongeza kuwa PULA inakwenda kuifanyaTanzania kama kitovu katika uwekezaji inaokwenda kupanua katika nchi zingine jirani kama Malawi .

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals