[Latest Updates]: Madini Vision 2030 kutangazwa Indonesia

Tarehe : Sept. 20, 2023, 3:56 p.m.
left

Ushirikiano Tanzania, Indonesia waimarishwa

 Madini ya Kimkakati kupewa kipaumbele

 Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo  Jatmiko amesisitiza kushirikiana na Tanzania katika kutangaza Mwelekeo Mpya wa Wizara wa VISION 2030: Madini  ni Maisha na Utajiri ili kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini Nchini.

Balozi Jatmiko amesema hayo  leo Septemba 20, 2023 jijini Dodoma  mara baada ya mazungumzo mafupi na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali katika kikao kilicholenga kujenga mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika shughuli za uchimbaji madini 

“Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimbali mbalimbali za madini ambazo ni muhimu na zinahitajika duniani. Kupitia Dira hiyo Sekta ya Madini inakwenda kutangaza nchini Indonesia na kueleza wawekezaji fursa mbalimbali zilizopo,” amesema Mhe. Jatmiko.

Ameongeza kuwa, kutokana na mahitaji makubwa ya matumizi ya nishati hiyo hususan magari ya umeme katika nchi hiyo, Serikali ya Indonesia itaweka vipaumbele katika matumizi ya madini mkakati kutoka nchini Tanzania ili waweze kukidhi mahitaji yao katika matumizi mbalimbali ya vifaa vya umeme.

Katika hatua nyingine, amempongeza Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde kwa kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Madini. Amesema nchi hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha nchini ili kuvutia  uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amesisitiza nchi hiyo kutoa ushirikiano katika kuwajengea uwezo wataalam mbalimbali wa wizara na taasisi katika maeneo ambayo yatahitajika ikiwemo mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini na mafunzo maalum kwa wakufunzi wachache  ambao watakuwa walimu katika kutoa mafunzo maeneo muhimu.

Pia, ameeleza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini ikiwemo ushirikiano katika uchimbaji wa madini ya dhahabu na madini ya kimkakati. ‘’Tunahitaji ushirikiano katika maeneo ya uchimbaji wa madini hayo kupitia Shirika la Madini la Taifa STAMICO na sisi Serikali tutatoa ushirikiano ili uchimbaji wa madini hayo ufanyike hapa nchini,” amesema Mahimbali.

Vile vile, amewakaribisha kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini linalotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26 mwaka huu. Amesema jukwaa hilo litatangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Kikao hicho kifupi kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga pamoja na wataalam mbalimbali wa Wizara.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals