[Latest Updates]: Tume ya Madini Kutoa Mafunzo Kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini Kuhusu Masuala ya Usalama na Usimamizi wa Mazingira

Tarehe : Nov. 16, 2020, 11:40 a.m.
left

  • Kukutanisha wachimbaji wadogo wa mikoa ya kimadini ya Mbeya, Chunya na Songwe

Tume ya Madini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira inatarajia kufanya mafunzo ya siku tatu kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa mikoa ya kimadini ya Mbeya, Chunya na Songwe ambapo yanatarajiwa kufanyika mjini Chunya Mkoani Mbeya.

Akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Dkt. Abdulrahman Mwanga amesema kuwa mafunzo hayo yanayotarajiwa kuanza tarehe 19    hadi tarehe 21 Novemba, 2020 yanalenga kuwapa wachimbaji wadogo wa madini uelewa mpana kuhusu masuala ya usalama, afya, utunzaji wa mazingira na usafirishaji na matumizi sahihi ya baruti kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

“Aidha elimu kuhusu sheria ya madini pamoja na kanuni zake itatolewa kwa wachimbaji wa madini kupitia wataalam waliobobea kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini,” amesisitiza Dkt. Mwanga.

Dkt. Mwanga ameeleza kuwa mafunzo husika yanatarajiwa kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila na kusisitiza kuwa mafunzo hayo ni  mwendelezo wa mafunzo kama haya yaliyofanyika katika mikoa ya Singida, Katavi na  Manyara ambapo yataendelea kutolewa katika mikoa  mingine ya kimadini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals