[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yabainishwa Mikakati ya Mikakati ya Kupambania na Magonjwa Ambukizi Migodini

Tarehe : Aug. 29, 2024, 11:28 a.m.
left

Dodoma

Imeelezwa kwamba kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi Agosti 2024 , Wizara ya Madini imeendelea  kuratibu na kusimamia  Masuala yanayohusu Usalama Mahali pa kazi pamoja na afya za wafanyakazi katika migodi ikiwemo UKIMWI , Kifua Kikuu na magonjwa sugu.

Hayo yamebainishwa Agosti 29, 2024 na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Madini Festus Mbwilo kwa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Mbwilo alieleza kwamba, katika kipindi husika, Wizara iliratibu Upimaji wa Kifua Kikuu na magonjwa sugu yasiyo ambukiza ambapo jumla ya watu 396 walipima, kati ya hao 184 ni wafanyakazi na 212 ni jamii inayozunguka mgodi.

Akielezea kuhusu mkakati wa Wizara Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa alisema, Wizara inaendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa mkakati wa  masuala ya UKIMWI na magonjwa yasioambukizwa katika migodi mikubwa na ya Kati ili kupunguza maambukizi  mapya na kuimarisha  nguvu  kazi ya wafanyakazi na jamii kama mkakati wa sekta ya madini unavyoelekeza kuhusu kudhibiti maambukizi ya UKIMWI , Kifua Kikuu na Magonjwa sugu.

Dkt.Kiruswa aliongeza kuwa, mkakati mwingine ni kushulika na vichochezi vya kijamii na kimfumo dhidi ya VVU kwa kutumia minutes za ushirikishwaji katika maeneo ya ndani na nje ya midogo sambamba na wachimbaji wadogo ambao wao wapo katika hatarishi zaidi kutokana uchimbaji wa kuhamahama.

Dkt.Kiruswa aliongeza kuwa , ili kuendelea kupambana na maambukizi ya VVU na magonjwa sugu, Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi zinazoshughulika na afya kubuni mbinu mpya rafiki katika kutoa elimu ya afya na kuzikumbusha kampuni za uchimbaji madinib ziendelee kuchangia mfuko wa kupambana na maradhi.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI , Bernadetha Mshashu aliipongeza Wizara ya Madini kwa kazi nzuri inayofanya ikiwa pamoja na kutekeleza maagizo yanayotolewa na Kamati kuhusiana na ujumuhishaji wa jamii ndani na nje ya migodi katika kutoa elimu ya afya. 

Naye, Daktari Aalen Mtemi alizungumza kwa niaba ya mgodi wa Uchimbaji dhahabu Geita (GGM) alisema, mgodi wa GGM unatambua umuhimu wa afya ya mfanyakazi mahali pa kazi hivyo katika kipindi husika imeweza kuchangia shilingi bilioni 1.75 katika Mifuko ya Kupambana na Maradhi yasioambukizwa na yanayoambukizwa.

Naye, Mwenyekiti kutoka Chama cha Wachimbaji Wanawake Mirerani, Recho Njau aliishukuru Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa jinsi  inavyotoa huduma za afya kupitia Mamlaka za afya kwa wachimbaji wadogo  Mirerani ikiwa pamoja na kutoa elimu ya afya kuhusiana na  magonjwa yanayotokana na shughuli za uchimbaji madini ikiwemo Kifua Kikuu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals