[Latest Updates]: Wizara ya Madini , Wafanyabiashara wa Baruti Wajadili Changamoto

Tarehe : May 18, 2024, 9:13 a.m.
left

Dodoma

Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga ameongoza kikao kazi cha wataalam wa Wizara, Tume ya Madini na wawakilishi wa Umoja Wafanyabiashara wa Baruti Tanzania  (TEDA)  kilicholenga  kujadili changamoto zinazohusiana na biashara ya baruti nchini.

Kikao hicho kilichofanyika   leo Mei 18, 2024 katika Ofisi za Wizara  jijini Dodoma, kimetumika kupokea  changamoto, maoni, mapendekezo na ushauri kutoka kwa Umoja huo  ambapo pia Wizara imekitumia  kujibu baadhi ya hoja  zilizowasilishwa huku nyingine zikipokelewa kwa ajili ya kuendelea kufanyiwa kazi.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Mwanga ameupongeza Umoja huo kwa kuona umuhimu wa  kukutana na Wizara ili kujadili kwa pamoja  masuala mbalimbali yanayohusu biashara ya baruti nchini na kueleza kuwa, vikao kama hivyo vitasaidia kujenga mahusiano mazuri  ikiwemo kubaini mapungufu na changamoto katika utekelezaji wa Sheria, Kanuni na taratibu mbalimbali zinazosimamia biashara ya baruti. 

" Sote tunafahamu bila biashara ya baruti hakuna uchimbaji, ninawapongeza kwa kuona umuhimu wa kukutana na sisi kujadili kwa pamoja changamoto zenu na nina amini vikao hivi vitakuwa chachu ya kufanya maboresho yanayofaa kwa Maendeleo ya Sekta hii," amesema Dkt. Mwanga.

Kwa upande wake, Katibu  Mtendaji wa  TEDA Mhandisi Gideon Kasege  akizungumza katika kikao hicho ameipongeza Serikali kwa kuandaa Kanuni za Baruti  ambazo zimeruhusu wauzaji wengi ikiwemo usafirishaji wa baruti.

Pamoja na hayo, Mhandisi Kasege ametoa angalizo kwa Serikali kuendelea na udhibiti wa biashara hiyo ambayo inaelezwa kuwa miongoni mwa bidhaa hatarishi.

Pamoja na masuala mengine yaliyowasilishwa, umoja huo umetoa ombi kwa Wizara la kuwa na mfumo wa vibali  vya baruti kwa njia ya mtandao ili kuondoa changamoto za upatikanaji wake.

Wizara ya Madini imekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto zinazokabili kila makundi ikiwemo wachimbaji wakubwa na wa kati, wachimbaji wadogo wa madini ya aina mbalimbali, watoa huduma migodini na wafanyabiashara wa madini   kwa lengo la kujadili changamoto, kupokea maoni, ushauri na mapendekezo kwa lengo la  kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.

Kikao hicho kimeazimia kukutana kila robo mwaka. 

Jukumu la utoaji wa leseni ya biashara ya baruti ni moja ya shughuli zinazofanywa na Wizara ya Madini Makao Makuu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals