Tarehe : March 27, 2019, 2:57 p.m.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewapongeza wakandarasi kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
Ametoa pongezi hizo leo tarehe 27 Machi, 2019 mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo na kuonesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.
“Nimefurahishwa sana na wakandarasi waliochukua zabuni za kujenga majengo ya ofisi hizi, hivyo ninawaomba Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) watoe vyeti kwenye majengo ambayo yamekamilika kwa asilimia mia ili waanze kutumia majengo hayo kama ilivyokusudiwa,” alisema Majaliwa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa hakuridhishwa na ubora wa milango iliyopachikwa kwenye jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Jengo la Wizara ya Fedha na kuagiza milango hiyo kubadilishwa.
Pia, Majaliwa ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka umeme mkubwa katika eneo hilo kwa wakati ili majengo yakamilike kwa asilimia mia na kufikia azma ya Serikali ya kuhamia katika mji wa Serikali baada ya ofisi hizo kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Mgufuli.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha, Philip Mpango, amesema mradi wa ujenzi wa nyumba hizo umezalisha ajira kubwa kwa vijana kutokana na kuajiri takribani watu 1141 walioshiriki katika ujenzi huo.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amesema jengo la Wizara limekamilika kwa asilimia 99, na kubainisha kuwa, mkandarasi yupo katika hatua za mwisho ili aweze kukabidhi jengo hilo.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.