[Latest Updates]: Serikali Kununua Mitambo Kumi ya Uchorongaji Kwa Ajili ya Wachimbaji Wadogo

Tarehe : May 17, 2024, 10:18 p.m.
left

Rais Samia aelekeza mitambo miwili kwa ajili ya wakina Mama na Vijana

Waziri Mavunde agawa Leseni kwa wakina Mama wachimbaji Dutwa-Simiyu

Awataka STAMICO kuendelea kuwasimamia na kuwaendeleza wachimbaji wadogo_

-RC Nawanda aahidi kusimamia utekelezaji wa mradi wa umeme migodini

Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imepanga kununua mitambo mingine 10 ya uchorongaji kwa ajili ya kusaidia wachimbaji wadogo nchini.

Hayo yamesemwa leo  17 Mei, 2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde aliposhiriki zoezi la kuwakabidhi leseni Chama cha Wanawake Wachimbaji Mkoani Simiyu (TAWOMA) katika Kata ya Dutwa Wilayani Bariadi.

"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha za kuongeza mitambo mingine 10 ya uchorongaji kupitia STAMICO na ametuelekeza kuwa mitambo hiyo ikifika nchini Mwezi Agosti au Septemba, 2024 mitambo 2 tuiweke mahsusi kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanawake na vijana" amesema Waziri Mavunde 

Ameongeza kwamba ni  dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuwawezesha wachimbaji madogo kwa kuwapatia vifaa na kuimarisha shughuli zao ili ziwanufaishe watanzania.

Pia, Waziri Mavunde amwmwagiza Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Mayigi  Makolobela kusimamia vijana na wanawake ili waunde vikundi, ili katika maeneo yanayorejeshwa Serikalini kwa zoezi la ufutaji wa leseni vikundi hivyo vipatiwe maeneo ya uchimbaji.

Akisoma risala kwa niaba ya Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA) mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa TAWOMA Taifa, Bi. Semeni Malale ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kuwawezesha wachimbaji wanawake nchini kuendesha shughuli zao na pia kumshukuru Ndg Emmanuel Silanga”Gungu” kwa kutoa Leseni hiyo kwa wakina mama wa Mkoa wa Simiyu.

Pia, panoja na mambo mengine, Bi. Semeni ametoa wito kwa wanawake wenzake kuchangamkia fursa hiyo ya uchimbaji baada ya kupokea leseni hiyo, huku akiiomba Serikali kuendelea kusaidia baadhi ya changamoto katika eneo la uchimbaji la Dutwa ikiwemo maji na barabara.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mhe  Dkt. Yahaya Nawanda ameishukuru Serikali kwa namna inavyosimamia sekta ya madini, na kuahidi kwamba ataendelea kutoa ushirikiano kwa akina mama na vijana wachimbaji madini ili shughuli zao ziendelee kuwanufaisha na kuchangia katika ustawi wa uchumi wa Mkoa wa Simiyu.

Akijibu changamoto za TAWOMA katika eneo la Dutwa, Mhe. Dkt. Nawanda amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Simon Simalenga kuhakikisha anasimamia suala la kuboresha barabara na kuleta maji katika eneo hilo la uchimbaji, kwani Serikali imeshaleta zaidi ya bilioni 4 Mkoani Simiyu kwa ajili ya uboreshaji barabara na mtandao wa maji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals