[Latest News]: Mapinduzi STAMICO Yaleta Manufaa kwa Umma Nchini

Tarehe : Aug. 29, 2023, 8:54 a.m.
left

*Yawashirikisha Watu wenye  mahitaji maalum katika shughuli za uchimbaji madini 
*Yajipanga kuwainua wachimbaji wadogo 

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesema litaendelea kusimamia miradi yake kikamilifu ili kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali madini.

Hayo yamesemwa August 28, 2023 na Dkt. Venance Mwasse Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo wakati wa Mkutano wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, STAMICO, na Wahariri wa Vyombo vya habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano cha Julius Nyerere  (JNICC) ambapo amebainisha kuwa kwa sasa Shirika hilo linasimamia miradi mbalimbali ikiwemo, Mradi wa Kiwira wa uchimbaji, uchakataji na uuzaji wa makaa ya mawe Mkoani Songwe.

Aidha ameeleza kuwa,miradi mingine inayosimamiwa na Shirika hilo ni pamoja na Mradi wa Mkaa Mbadala wa kupikia kwa kutumia makaa ya mawe, Mradi wa Dhahabu STAMIGOLD unaomilikiwa na serikali kwa hisa asilimia 99 na Msajili wa Hazina hisa asilimia 1 pamoja na kiwanda cha kusafisha Dhahabu Mwanza ambacho kinamilikiwa na Shirika hilo kwa asilimia 25 na Mbia asilimia 75. 

"Uanzishwaji wa kiwanda hicho umesaidia, kusafisha dhahabu na mazao ambatano, uhaulishaji wa Teknolojia, kuongeza huduma kwa Jamii (CSR), mapato kwa serikali, STAMICO, na Serikali za Mitaa, kuongeza ajira, kupunguza utoroshaji wa dhahabu,
kutambulika kimataifa na kuimarisha Shilingi ya Tanzania na Uchumi." Amesema Dkt. Mwasse

Mkurugenzi huyo pia amebainisha kuwa kwa sasa Shirika hilo limeongeza thamani yake na kuwezesha Taasisi mbalimbali zilizo chini yake kuendelea kufanya vyema kutokana na usimamizi mzuri wa sera na miongozo mbalimbali ya serikali kuhusiana na sekta ya madini.

"STAMICO Kutoka Shirika linalotengeneza hasara hadi Shirika linalotengeneza faida, tumeweza kulipa gawio kwa serikali jumla ya Shilingi Bilioni 8, tumeondokana kabisa   na utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini, tumepata hati safi kwa miaka 3 Mfululizo kutokana na ukaguzi wa Mahesabu, lakini pia Mapato ya ndani yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 1.3 kwa Mwaka 2018/19 hadi Shilingi Bilioni 61.1 kwa mwaka 2022/23." Amefafanua Dkt. Mwasse.

Vilevile amesema kwa sasa STAMICO imeendelea kuwainua wachimbaji wadogo kwa kuwafundisha mambo mbalimbali yanayohusiana na uchimbaji, ikiwemo masuala ya kisheria, na teknolojia.

"Tulifanya utafiti kwa wachimbaji wadogo na kubaini wana changamoto mbalimbali zikiwemo, elimu ya uchimbaji, ukosefu wa taarifa sahihi za mapato, Teknolojia duni, kutokuwa na mitaji/kutokukopesheka, na ukosefu wa masoko ya bidhaa zao.", hivyo basi Shirika limeanzisha vituo vya mfano vya kujifunzia teknolojia vyenye tija ya uchimbaji katika maeneo ya Lwamgasa, Katente na Itumbi, pia tumeongeza uwezo wa kutoa huduma katika vituo hivyo na kutekeleza makubaliano (MOU) na Taasisi za kifedha CRDB, NMB, AZANIA na KCB ili ziweze kuwakopesha
 mitaji wachimbaji wadogo na kuwawezesha safari za kujifunza ndani na nje ya nchi. Amesema Dkt Mwasse

Aidha STAMICO kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), wameingia makubaliano ya awali na Kampuni za GF Truck na Apolo ili kuwawezesha kupata Vifaa kutoka kwa kampuni wauzaji wa Mitambo ya uchimbaji madini.
 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals