[Latest Updates]: Dondoo za Bajeti Kuu ya Serikali, Sekta ya Madini

Tarehe : June 13, 2024, 10:44 p.m.
left

BAJETI KUU YA SERIKALI

#Sekta ya Madini

"Katika kipindi cha Awamu ya Sita kumekuwa na mafanikio katika Sekta ya Madini ikiwemo kuendelea kuongezeka kwa mchango Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kutoka asilimia 7.3 mwaka 2021 hadi asilimia 9.0 mwaka 2023," Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

BAJETI KUU YA SERIKALI

Sekta ya Madini

"Kuongezeka kwa vituo vya ununuzi wa madini kutoka 61 Mwaka 2020/21 hadi vituo 100 mwaka 2023/24; pamoja na kuanzishwa kwa soko jipya moja (1) la madini hivyo kufikia masoko 42. 


BAJETI KUU YA SERIKALI

#Sekta ya Madini

"Serikali imenunua mitambo mitano (5) ya uchorongaji kwa ajili wachimbaji wadogo inayotumika katika maeneo mbalimbali nchini," Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

BAJETI KUU YA SERIKALI

#Sekta ya Madini

"Serikali kupitia Benki Kuu ya  Tanzania imeanzisha utaratibu wa kununua dhahabu kwa ajili ya akiba ya Taifa (National Gold Reserve) kwa lengo la kuimarisha akiba ya fedha za kigeni na kusaidia katika utekelezaji wa Sera ya Fedha. Hadi Aprili 2024, Benki Kuu ya Tanzania imenunua dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani milioni 26 ambapo malengo ya Serikali ni kununua tani sita (6) za dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani milioni 400," Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba

BAJETI KUU YA SERIKALI

#Sekta ya Madini

"Serikali inaendelea
kuhamasisha viwanda vya ndani vya kuchenjua dhahabu kufanya taratibu za kupata Ithibati ya London Bullion Market Association (LBMA) ili kuwezesha dhahabu inayosafishwa kutambuliwa kwenye masoko ya kimataifa na kuweza kununuliwa kwa ajili ya kuhifadhiwa kama fedha"Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals