[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Atatua Mgogoro wa Zaidi ya Miaka Minne Chunya

Tarehe : Dec. 16, 2024, 7:19 p.m.
left

Tume ya Madini yaelekezwa kusimamia utekelezaji wa makubaliano
 
Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanikiwa  kutatua mgogoro uliodumu zaidi ya miaka minne kati ya familia ya Tibe Rwakatare ambao ni wamiliki wa Leseni ya uchimbaji  mdogo  wa Madini na Juma Kasola ambaye ni mmiliki wa eneo la ardhi lenye ukubwa wa  Hekari 9 katika Wilaya ya  CHUNYA Mkoa wa Mbeya.
 
Mgogoro huo umetatuliwa leo Desemba 5,2024 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa katika kikao cha utatuzi wa mgogoro huo kilichofanyika katika ukumbi wa Abdulkarim  Mruma Dodoma baada ya majadiliano na pande zote mbili.
 
Aidha, katika kikao hicho Tibe Rwakatare alikubaliana na azimio la kurejeshewa ada zote za leseni walizolipia tangu kutolewa kwa leseni husika na  Juma Kasola ifikapo Januari 5, 2025 ili aachie eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 9 kwa Juma Kasola mara  baada ya kurejeshewa gharama hizo.
 
Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amezitaka pande zote mbili kuhakikisha zinatekeleza makubaliano hayo na Tume ya madini kusimamia utekelezaji wa mchakato huo kwa mujibu wa sheria ili kulinda haki za pande zote mbili.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals