[Latest Updates]: Wizara ya Madini, Tume ya Madini na BoT Wakutana na Wadau wa Madini

Tarehe : Oct. 4, 2024, 1:50 p.m.
left

Ikiwa ni mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa madini kuhusu utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini Sura 123
 
WIZARA YA MADINI, TUME YA MADINI NA BOT YAKUTANA NA WADAU WA MADINI
 
DODOMA
 
Ikiwa ni mkakati wa kujenga uelewa kwa wadau wa madini kuhusu utekelezaji wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini Sura 123, leo Oktoba 04, 2024 Wizara ya Madini imeratibu mkutano wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini uliofanyika jijini Dodoma ambapo elimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo imetolewa na wataalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
 
Viongozi walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Kamishna Msaidizi – Uendelezaji Migodi, Mhandisi Ally Samaje aliyemwakilisha Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, Meneja wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Lameck Kakulu, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki na watendaji wengine kutoka Tume ya Madini.
 
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, Kamishna Msaidizi – Uendelezaji Migodi kutoka Wizara ya Madini, Mhandisi Ally Samaje amesema kuwa lengo la maboresho ya sheria hiyo inayomtaka kila mchimbaji na mfanyabiashara wa madini kutenga angalau asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa kwa ajili ya kuisafisha hapa nchini na kuiuzia BoT kabla ya kuisafirisha nje ya nchi ni kuimarisha uchumi wa nchi na kuongeza akiba (reserve) ya dhahabu nchini.
 
Ameendelea kusema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wachimbaji na wafanyabiashara wa madini wanafanya kazi katika mazingira mazuri pasipo kuathiri biashara zao.
 
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo ameongeza kuwa sababu nyingine ya maboresho ya sheria hiyo ni kuhamasisha mnyororo wa shughuli za madini kufanyika nchini kuanzia kwenye uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji na biashara ya madini.
 
Wakati huohuo, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina sambamba na kuipongeza Serikali kwa maboresho ya Sheria za Madini ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuendelea kuangalia namna bora ya kuwawezesha watanzania kushiriki katika Sekta ya Madini na kuendelea kutatua changamoto  wanazokabiliana nazo wadau wa madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals