[Latest Updates]: Wizara ya Madini na Kampuni ya Barrick Zaanza Mikakati ya Kuwaandalia Mazingira Rafiki Wachimbaji Wadogo

Tarehe : Oct. 5, 2024, 1:56 p.m.
left

●Kufanya utafiti katika maeneo yenye leseni.

KAHAMA

Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni ya  Dhahabu ya Barrick zinatarajia kuanza mikakati ya kufanya utafiti katika maeneo yenye leseni mkoani Mara yatakayotumiwa na wachimbaji wadogo wa madini baada ya utafiti kukamilika ikiwa ni lengo la kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo ili wachimbe kwa tija.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 5,2024 na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Mkutano wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji ya Robo Mwaka ya kampuni ya Barrick mkoani Shinyanga.

Dkt.Kiruswa amesema kuwa, kwa kipindi kirefu Mgodi wa North Mara  umekuwa na changamoto ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo unaoambatana na uharibifu wa mali ambapo kupitia majadiliano ya pamoja tumekubaliana kuunda timu itakayofanya tafiti katika leseni 13 na baadae kuyakabidhi kwa wachimbaji wadogo kwa utaratibu maalum utakaojumuisha ngazi mbalimbali za kiutendaji.

Dkt.Kiruswa amesema, Kampuni ya Barrick imekuwa na mchango mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo Serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa migodi yote  kuendelea  ili shughuli za uchimbaji zifanyike kwa usalama pamoja na wachimbaji wadogo kupata maeneo mazuri ya uchimbaji.


 Akielezea kuhusu timu ya utafiti Dkt.Kiruswa ameeleza kuwa,  makubaliano ya awali  ni kuunda timu  itakayojumuhisha wataalam kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini, Kampuni ya Barrick , Uongozi wa Mkoa , wawakilishi wa wachimbaji wadogo ambapo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 15, 2024 jijini Dodoma.

Kwa upande wake , Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya  Barrick , Mark Bristow amesema kuwa utafutaji wa madini unaoendelea katika maeneo yaliyotumika na kuachwa kwenye migodi ya Bulyanhulu na North Mara unaendelea ambapo tayari maendeleo mazuri yanayoweza kuongeza migodi mipya kwa Barrick.

Akielezea kuhusu michango ya Barrick kwa jamii Bristow amesema , kupitia mpango wa Bartick na Twiga  wa kusongesha mbele Sekta ya Elimu tayari mpaka sasa ujenzi wa shule zipatazo 64 zikiwa na thamani ya dola milioni 10, ikiwa pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 396, mabweni 97 yamejengwa.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi amezipongeza kampuni ya Twiga na Barrick kwa juhudi za maendeleo kwa jamii inazofanya kupitia Mpango wa Ushirikishwaji wa jamii inayozunguka mgodi hususani katika Sekta  ya Elimu , Miundombinu ya Barabara na Ujenzi wa Vituo  vya Afya.

Sambamba na hapo, katika kutambua juhudi zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali kampuni za Twiga na Barrick zimetoa kiasi dola za Marekani elfu 30 kwa asasi na mashirika  ya kijamii.

Mkutano huo umejumuisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya mkoa , wilaya , kata na vitongoji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals