[Latest Updates]: Dkt. Biteko: Barabara na Umeme Kupelekwa kwenye Viwanda vya Chumvi Bagamoyo

Tarehe : July 18, 2023, 10:12 a.m.
left

Bagamoyo inazalisha chumvi tani elfu 90 hadi tani laki moja kwa mwaka

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema Serikali imekusudia kuweka mazingira wezeshi kwenye sekta ndogo ya chumvi ambapo tayari imeshapata mkandarasi wa kutengeneza barabara kwa lengo la kuongeza tija kwenye uzalishaji wa madini ya chumvi na pia, serikali imekamilisha taratibu za kupeleka nishati ya umeme Bagamoyo kitu ambacho kitaongeza uzalizalishaji zaidi wa madini hayo.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Julai 18, 2023 alipofanya ziara katika Viwanda vya kuzalisha chumvi vya Sea Salt  na Stanley vilivyopo katika eneo la Saadani wilaya ya Bagamoyo.

Aidha, Dkt. Biteko amesema takwimu za Wizara ya Madini zinaonesha kwamba eneo la Bagamoyo mkoani Pwani linazalisha kati ya tani elfu 90 hadi tani laki moja za madini za chumvi kwa mwaka ambapo bado kuna uhitaji wa kuzalisha zaidi kutokana na uwepo wa pwani ndefu zaidi kuliko nchi nyingine za jirani.

Dkt. Biteko amesema, katika kuhakikisha uzalishaji wa madini ya chumvi unaimarika nchini, serikali imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya uzalishaji wa chumvi kwa kuzuia uagizaji wa chumvi ghafi kutoka nje ya nchi, kupunguza tozo na kodi zilizokuwepo kwenye sekta ndogo ya chumvi.

"Kama mnavyofahamu serikali ilikuwa inatoza zaidi ya tuzo 17 ambapo kwa sasa serikali imezipunguza na kubaki tozo nane lakini vilevile mrabaha wa chumvi ulikuwa asilimia tatu serikali imepunguza mpaka asilimia moja," amesema Dkt. Biteko.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Biteko ametoa wito kwa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuangalia tozo wanazotoza kwenye sekta ya chumvi ziwe rafiki ili zisiwaongezee mzigo mkubwa wazalishaji wa madini hayo, ambapo amesema nchi za jirani bei ya chumvi iko chini kutokana na gharama za uzalishaji kuwa chini zilizosababishwa na uwepo wa miundombinu mizuri na upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Stanley, Richard Stanley amempongeza Dkt. Biteko kwa kufanya ziara katika eneo hilo ambapo ameeleza kuwa changamoto kubwa inayoikabili Sekta ya Ndogo ya Madini ya Chumvi katika eneo la Bagamoyo ni ukosefu wa masoko ya bidhaa hiyo, miondombinu ya barabara ambayo kipindi cha masika haipitika kiurahisi pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme.

Naye, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Ally Maganga amesema ofisi yake itaendelea kutatua changamoto zilizopo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, kuongeza ajira, kuongeza mapato ya serikali na kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals