[Latest Updates]: Mgodi wa Kiwira - Kabulo Wapanga Kuzalisha Tsh. Bilioni 40 kwa Mwaka

Tarehe : Aug. 21, 2023, 8:10 a.m.
left

GST kushirikiana na STAMICO kuchunguza ubora wa sampuli

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amepokea taarifa kuhusu mpango wa Mgodi wa Kiwira-Kabulo unaomilikiwa na Shiriki la Madini la Taifa (STAMICO) kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 ni kuzalisha Makaa ya Mawe yenye thamani ya shillingi bilioni 40.

Dkt. Kiruswa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mratibu wa Mgodi wa Kiwira-Kabulo Mhandisi Peter Maha wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio, changamoto na mipango ya Mgodi katika Mwaka wa Fedha 2023/24.
 
Ili kutekeleza hilo, Dkt. Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kushirikiana na STAMICO katika uchungizi wa sampuli za Maabara hususan katika kuchunguza ubora wa Makaa ya Mawe.

Ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea mgodi wa Kiwira-Kabulo uliopo katika Kijiji cha Kapeta Kata ya Ikinga wilayani Ileje mkoa wa Songwe ambapo amesema GST tayari ina Ithibati inayotambulika Kimataifa hivyo Taasisi hizo mbili zishirikiane kupima ubora wa Makaa hayo mgodini hapo ili kupunguza asumbufu kwa wateja wanaotaka kupata vipimo kutoka Maabara zilizo thibitishwa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Kiruswa amesema, kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika mgodi wa Kiwira-Kabulo, ni vyema akatafutwa mwekezaji mkubwa Ili ashirikiane na STAMICO katika uchimbaji wa makaa ya mawe ambapo kwa sasa yanahitajika kwa wingi katika nchi mbambali duniani ili kuongeza uzalishaji na kuchimba kwa faida kwa lengo la kunufaisha uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kiruswa ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kufanya vizuri katika uzalishaji wa makaa ya mawe na kuendelea kuchangia huduma kwa jamii zinazozunguka mgodi kama Sheria zinavyoelekeza na pia, amewasihi watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujitoa ili kuandika historia mpya kati ya miradi ya STAMICO iliyofanikiwa.

Pia, Dkt. Kiruswa ameahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi huo ikiwemo upungufu wa wafanyakazi, vitendeakazi, madai ya watumishi na uchakavu wa majengo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mgodi wa Kiwira-Kabulo Mhandisi Maha amemshukuru Naibu Waziri kwa kufanya ziara katika mgodi huo ambapo amesema kitendo hicho kitaongeza morali ya kazi na kuchochea maendeleo ya uzalishaji katika mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kuendeleza uzalishaji wa makaa ya mawe na kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals