[Latest Updates]: Kamati ya Nishati na Madini Yapongeza Mendeleo Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini

Tarehe : Aug. 12, 2024, 12:58 p.m.
left

●Ujenzi wa Jengo wafikia asilimia 84.4

Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt.Mathayo Mathayo amepongeza maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Madini awamu ya pili kwa juhudi mbalimbali zinazofanyika na kupelekea kufikisha  asilimia 84.4 ya ujenzi katika mji wa Serikali Mtumba. 

Dkt. Mathayo ametoa pongezi hizo leo Agosti 12 , 2025 jijini Dodoma  wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo awamu ya pili linaloendelea kujengwa katika wa Mji wa  Serikali Mtumba.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu, Festus Mbwilo amesema mpaka kufikia  Agosti 2, 2024 utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo la ghorofa  tano ulifikia asilimia 84.4 na sehemu iliyobakia ni asilimia 15.6.

Awali, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  amesema kuwa utekelezaji wa mkataba ulikuwa miezi 18 lakini kutokana na changamoto mbalimbali mkandarasi hakuweza kukamilisha kwa wakati ambapo tarehe ya mkataba ya awali  kukamilisha jengo ilikuwa Aprili 14, 2023.

Akielezea kuhusu changamoto zinazojitokeza katika ujenzi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizara ya madini Augustine Ollal amesema kumekuwepo na mabadiliko ya mifumo hususani mifumo ya zimamoto ambayo inapelekea mkandarasi kusubiri maelekezo yanayojumuisha wizara zote kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ili kukamilisha ujenzi.

Ollal ameongeza kuwa changamoto nyingine ni kuchelewa kwa vifaa kulikosababishwa na upungufu wa fedha za kigeni katika  manunuzi nje ya nchi.

Sambamba na Mhe.Waziri kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Mhandisi Yahya Samamba , Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo pamoja na maafisa mbalimbali kutoka wizara ya madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals