[Latest Updates]: Mataifa ya Afrika Mashariki Yatakiwa Kushirikiana Katika Kuongeza Thamani Madini

Tarehe : Nov. 20, 2024, 12:57 p.m.
left

Asema matamanio yake ni kuona kunapatikana mabilionea kupitia sekta ya madini

Akiri Tanzania kuwa kinara wa Sekta ya Madini Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 

Waziri wa Madini na Uchumi wa Buluu wa Kenya, Mhe. Ali Hassan Joho, ametoa wito kwa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana kwa karibu katika kuongeza thamani ya madini yanayopatikana ndani ya ukanda huo. 

Waziri Joho alitoa kauli hiyo leo Novemba 20, 2024, akiwa Mgeni Rasmi katika Hafla ya Usiku wa Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

“Tunapaswa kushirikiana kuhakikisha madini yanayotokana na nchi zetu hayauzwi yakiwa ghafi, bali yanaongezewa thamani kabla ya kuingia kwenye masoko ya kimataifa, hii ni fursa kubwa kwetu” amesema Joho. 

Amesema kuwa, kutokana na uwepo wa rasilimali za madini katika ukanda wa Afrika Mashariki, matamanio yake ni kuona siku moja wanapatikana mabilionea wazawa wwanaotokanana shughuli za uchimbaji, usafishaji pamoja na biashara ya madini. 

Aidha, Mhe. Joho amesisitiza kuwa, kama Kenya wameona umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2024 kwa kuwa wamepata nafasi ya kujifunza mbinu bora za kuboresha Sekta ya Madini kupitia mijadala na mafanikio yaliyoanisha kupitia mijadala inayoendelea.

Mhe. Joho amebainisha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika Sekta ya Madini, hasa kupitia maboresho ya Sheria na  Sera za Madini na kuongeza kuwa “Hatua hizi zimebadili kabisa mwelekeo wa sekta hii hapa Tanzania na zinaleta fursa za kutengeneza matajiri wakubwa kupitia rasilimali zetu,” ameongeza Joho.

Tanzania ni kiranja wa Sekta ya Madini Afrika Mashariki

Kwa upande wake, Waziri wa Madini wa Tanzania, Mheshimiwa Anthony Mavunde, alisisitiza kuwa Tanzania imejidhihirisha kuwa nguzo ya sekta ya madini katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Tanzania ni powerhouse ya sekta ya madini. Uwekezaji wa kimkakati katika kuongeza thamani ya madini utaleta manufaa makubwa kwa uchumi wetu na jamii zetu kwa ujumla,” amesema Mavunde.

Ametaja manufaa hayo kuwa ni pamoja na Kuongeza Mapato ya Serikali kupitia kodi na ada za biashara zinazotokana na bidhaa zilizoongezewa thamani ni kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya kuongezewa thamani madini. 

Waziri Mavunde ameongeza manufaa mengine kuwa kulinda na kuongeza ajira kwa wazawa, kuimarisha Sekta ya Viwanda kwa kuchochea ukuaji wa viwanda vya ndani, kukuza uchumi wa ndani kwa kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya nchi sambamba na kuboresha biashara ya kimataifa kwa kuingia masoko ya kimataifa na bei za juu.

Uganda Yasifu Jitihada za Tanzania

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Madini kutoka Uganda, Mhe. Phiona Nyamutoro, amesifu mafanikio ya Tanzania katika sekta ya madini, hasa katika ukusanyaji wa mapato, mpango wa kuongeza thamani ya madini, na usimamizi bora wa sekta hiyo.

“Tanzania imeonyesha mfano mzuri wa jinsi ya kusimamia sekta ya madini kwa tija, jambo ambalo linafaa kuigwa na nchi zote za Afrika Mashariki,” amesema Nyamutoro.

Hafla ya Usiku wa Madini huambatana na onesho la bidhaa za madini ya vito sambamba na kutoa tuzo kwa wadau waliofanya vizuri katika sekta ya madini nchini Tanzania.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals