[Latest Updates]: Tanzania na Canada Kushirikiana Kwenye Kukuza Ujuzai wa Wadau Sekta ya madini

Tarehe : March 5, 2025, 2:45 p.m.
left

Watanzania kujengewa uwezo kwenye teknolojia ya uchimbaji na uchenjuaji madini

Vyuo vya VETA kutumika kutoa mafunzo maalum

Canada yaipongeza Tanzania kwa kukuza sekta ya madini

Mpango wa Uwezeshwaji wa Vijana na wakina mama waungwa mkono

Toronto, Canada.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mh. Ahmed Hussein na Waziri wa Madini wa Tanzania Mh. Anthony Mavunde wamefanya mazungumzo ya masuala mbalimbali ya kuboresha uhusiano baina ya nchi mbili hizo hasa katika eneo la kuwajengea uwezo wataalamu na wachimbaji wa madini nchini Tanzania katika matumizi ya teknolojia ya kisasa ya uchimbaji na uchenjuaji madini.

Mazungumzo hayo yamefanyika jana Toronto,Canada na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mh. Joseph Sokoine sambamba na wataalamu wa Wizara zote mbili.

Akitoa maelezo ya awali,Waziri Ahmed Hussein ameipongeza Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa namba ambayo imeweka mazingira mazuri ya ukuaji wa sekta ya Madini nchini na kwamba Canada itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania hasa katika eneo la kuwajengea uwezo wataalamu na wachimbaji madini kwenye matumizi sahihi ya teknolojia ya uchimbaji na uchenjuaji madini.

“Tumekuwa na miradi ya maendeleo ya elimu nchini Tamzania,hivyo kupitia vyuo vya mafunzo ya Ufundi itakuwa rahisi kuja na mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania,hasa wakina mama na vijana, kushiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzima wa sekta ya madini“Alisema Hussein

Kwa upande wake,Waziri Anthony Mavunde ameishukuru nchi ya Canada kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania na pia kubainisha uwepo wa Kampuni kubwa za Madini kutokea nchini Canada zimechochea kwa kiwango kikubwa maendeleo ya kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zitokanazo na uwekezaji huo.

“Tanzania hivi sasa tuna programu yenye lengo la kuwezesha ushiriki kamilifu wa wakinamama na Vijana kwenye sekta ya madini,hivyo kuwajengea uwezo wa kiujuzi kwenye mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya madini kutachochea kukua kwa kasi kwa sekta ya madini.

Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi vinaweza kutumika kutoa mafunzo maalum ya jamii husika kutokana na aina ya shughuli za madini katika eneo husika.

Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kwa Canada katika utelekezaji wa mpango huu wenye tija kwa nguvu kazi ya Taifa Tanzania.“Alisema Mavunde

Akitoa maelezo ya ziada,Balozi Joseph Sokoine ameikaribisha mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini Canada kuwekeza nchini Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la ujenzi wa miundombinu na kwenye sekta ya madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals