[Latest Updates]: Tume ya Madini yawakingia kifua wagunduzi wa madini

Tarehe : June 11, 2019, 5:18 a.m.
left

Na Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) Nachingwea

Kamishna wa Madini Prof. Abdulkarim Mruma, amezitaka serikali za mitaa hususani ofisi za wakuu wa wilaya kuwarasimisha maeneo wananchi wanaogundua madini katika mfumo usio rasmi mara baada ya wananchi hao wanapogundua madini kwa kuokota kwenye maeneo mbalimbali ili kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara baada ya wananchi hususani wachimbaji wadogo na kisha kuvamiwa na wachimbaji na wawekezaji wakubwa.

Prof. Mruma amesema hayo wakati wa mazungumzo baina ya Tume ya Madini chini ya Mwenyekiti wake Prof. Idris Kikula na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Nachingwea Rukia Muwango walipo mtembelea ofisini  kwake kwa mazungumzo, na hiyo ni mara baada ya kumalizia kikao cha awali kilicho ikutanisha baina ya viongozi wa juu wa tume ya madini na wafanyakazi wa tume hiyo mkoa wa Lindi kwenye ofisi zao zilizopo wilayani Nachingwea jana.

Prof. Mruma amesema serikali za mitaa zinawajibu wa kulinda haki ya wananchi wanaogundua madini kwenye maeneo mbalimbali nchi ili kuwapa umiliki kwa kuwatambua wenyewe binafsi na eneo ambalo madini hayo huokotwa kabla ya kwenda kwenye ofisi za maafisa madini wa kazi waliopo nchi nzima.

Amesema na kuongeza kuwa wananchi nao wanapogundua madini au kuokota katika maeneo yasiyo rasmi hatua ya kwanza wakimbilie kwenye ofisi za serikali za mitaa kwenda kuripoti na ofisi hizo mara moja ziwatambue watu hao na mahali walipogundulia ili wasiporwe na wajanja.

“Naziomba serikali za mitaa hususani ofisi za wakuu wa wilaya ziwarasmishe kwa kuwatambua wao wenyewe na eneo husika walilogundua madini hayo ili kuleta udhibiti wa eneo kwa kuwatambua wahusika mapema kabla ya mgogoro ya umiliki. Amesema mara nyingi inapotokea hali kama hiyo kumekuwa na uwezekano wa wananchi kuporwa haki ya umiliki wakati mwingine na vyombo vya serikali bila wao kujiju hasa inapogundulika kuwa na madini wenye nguvu hukimbia mara moja kukata leseni ya eneo hilo na kuanza kuwafukuza waliogundua au wakati mwingine hata kuandikwa leseni jina la mtu asiyejulikana ili apewe mwekezaji mkubwa.” amesema Prof. Mruma.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya amemshukuru prof. Mruma kwa kumpa elimu hiyo ambayo amesema ni muhimu kwani kwa kufanya hivyo inalinda haki ya mtu. Amesema hata Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anathimini wagunduzi wa madini ndio maana alitoa Milioni 100 kwa mgunduzi wa Tanzanite hivyo sisi pia tunao  wajibu wa kuwalinda kwa kuwarasmisha kwa kuwatambua wagunduzi hao ili maeneo hayo yasivamiwe na wajanja. 

Wakati huo huo Prof. Kikula na DC wamejadili changamoto ya uuzaji wa madini yanayopatika mbali na soko la Nachingwea ambapo imebainika kuwa wengi wao hupeleka Tunduru kuuzia madini yao. Katika kujadili wameona kuwa endapo kama wachimbaji hao hakuna sababu ya kuwazuia kwenda kuuza madini yao kwenye soko la Madini Tunduru linalotambuliwa na serikali, haina shida chamsingi ni kuandaliwa utaratibu utakao watambulisha wachimbaji hao na kupewa kibali ili mauzo yatakayofanyika soko la Tunduru kwa madini yaliyotoka Nachingea rekodi zake zipelekkwe Nachingwea na hilo linawezekana kwa kufanya mazungumzo baina ya Ofisi ya Tume ya Madini Tunduru na ile ya Nachingwea ili kuwaondolea usumbufu wachimbaji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals