[Latest Updates]: Naibu Waziri Biteko awataka wachimbaji wa jasi kuungana

Tarehe : April 28, 2018, 11:22 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka Wachimbaji wa Madini ya Jasi kuungana ili kuweza kuandaa Kanuni ndogo ndogo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto katika utekelezaji wa shughuli zao ikiwemo ya Bei ya Madini ya Jasi.

Aliyasema hayo tarehe 17 Januari, 2018, wakati alipowatembelea   Wachimbaji Wadogo katika ziara ambayo inalenga kutatua migogoro iliyopo katika sekta husika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Naibu Waziri alisema kuwa bei ya madini ya Jasi imekuwa ikitofautiana kutokana na kukosekana kwa umoja baina ya wachimbaji wa madini hayo.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Jasi, Peter Ludvick (wa tatu kushoto). Naibu Waziri amemweleza mwenyekiti huyo kuhusu umuhimu wa kuandaa Kanuni ndogo ndogo ambazo zitawasaidia wachimbaji wa madini hayo kukabiliana na changamoto ya Bei ya Madini ya Jasi.[/caption]

“ Jiungeni pamoja mpange bei ya kuuza Jasi kwa pamoja na mkiwa kitu kimoja changamoto hizi hazitakuwepo,” amesisitiza Biteko.

Pia, Naibu Waziri alisema kuwa, ameelezwa kuwa ipo changamoto ya miundombinu ya barabara na hivyo kuitaka Halmashauri ya Kilwa kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo   kwa kuwa  itatumka kwa  shughuli mbalimbali.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mayigi   Makolobela alisema kuwa Jasi inayochimbwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara ina ubora wa asilimia 89-95 na iko juu ukilinganisha na Jasi inayopatikana nchi  jirani.

Vilevile, Makolobela ameeleza kuwa kiwango cha Jasi kilichochimbwa katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba, 2017 kilikuwa Tani 44,500 na gharama yake ilikuwa Shilingi bilioni 4.6.

Aliongeza kuwa, katika kiasi hicho cha Jasi kilichopatikana Serikali imekusanya Mrabaha wa shilingi milioni 138 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2017.

Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Jasi Mkoa wa Lindi, Peter Ludvick alimweleza Naibu Waziri kuwa ikiwa Serikali itawasaidia  suala la miundombinu hususan  barabara wachimbaji watazalisha mara tatu ya kiwango wanachokizalisha hivi sasa.

Imeandaliwa na:

Rhoda James,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals