Tarehe : March 8, 2025, 3:09 p.m.
Nishati ya Rafiki Briquettes inayozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ndio muwezeshaji mkubwa wa nishati safi inayotumika hapa Mkoani Arusha kwenye usiku wa nyama choma leo Machi 07, 2025.
Tukio hili la uchomaji nyama linafanyika kwenye makutano ya barabara eneo la Clock Tower ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 8 Machi.
Kitaifa maadhimisho haya yanafanyika mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Ndugu Paul Makonda amevutiwa na nishati hii na kuahidi kuitumia katika matukio yote ya umma katika Mkoa huu.
Rafiki Briquettes ni nishati rafiki kwa mazingira na isiyokuwa na madhara ya kiafya kwa watumiaji kwani haitoi moshi kama ilivyo kwa mkaa unaotokana na miti pamoja na kuni.
Nishati hii ina uwezo wa kuivisha na kuchoma nyama na vyakula vinginevyo katika viwango stahiki.
Taasisi nyingi za elimu, Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinatumia nishati ya Rafiki Briquettes kupikia.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.