Tarehe : Aug. 10, 2018, 6:50 a.m.
Na Asteria Muhozya,
Waziri wa Madini Angellah Kairuki, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Longido pamoja na ujumbe aliombata nao wakati wa ziara yake mkoani Arusha, tarehe 9 Agosti,2018, alitembelea eneo la Mpaka wa Namanga, linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Anorld Kisheshi wakati akitoa ufafanuzi wa namna scanner katika eneo hilo zinavyofanya kazi.[/caption]
Waziri Kairuki alitembelea eneo husika kwa lengo la kukagua na kuangalia namna shughuli za udhibiti wa utoroshaji wa madini maeneo ya mipakani zinavyoendelea.
Waziri Kairuki alisema baada ya kufika eneo husika alikuta kuna suala la changamoto ya upungufu wa wafanyakazi na hivyo kuahidi kulifanyia kazi kwa haraka suala hilo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema changamoto katika eneo hilo ni upungufu wa wafanyakazi na kuongeza kuwa, tayari Waziri wa madini ameahidi kulifanyia kazi suala husika ili kudhibiti utoroshaji madini katika maeneo ya mipaka.
Aliongeza kuwa, tayari Serikali ya Wilaya imeanza kuweka alama kujua mipaka ya Tanzania katika eneo husika ikiwemo kufuatilia njia za panya ambazo zinaweza kutumika kutorosha madini nje ya nchi.
Naye Mkaguzi wa Migodi, Anold Kisheshi alisema kuwa, serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali kudhibiti utoroshaji wa madini katika maeneo ya mipaka.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.