[Latest Updates]: Madini ya Dhahabu Kilo 15.78 Yenye Thamani ya Tsh Bilioni 3.4 Yakamatwa Bandarini Yakitoroshwa

Tarehe : Sept. 11, 2024, 1:17 p.m.
left

●Watuhumiwa watatu wakamatwa_

●Waziri Mavunde asisitiza kufuta leseni zao za kufanya biashara ya madini

●Atoa rai kwa wadau kuzingatia sheria na taratibu

Dar es Salaam

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ametangaza kukamatwa kwa madini ya dhahabu kilo 15.78 bandarini yalipokuwa yakitoroshwa.

Waziri Mavunde amesema hayo leo tarehe 11 Septemba, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari.

"Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya  uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini. Sasa basi, tunapokuwa na watu wachache ambao wanajihusisha na vitendo vya utoroshaji wa madini kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia" amesema Mavunde

"Kilo hizo 15.78 kwa bei ya leo zina thamani ya takribani bilioni 3.4 fedha ambazo kwa sasa zote watoroshaji hawa wanakwenda kuzipoteza. Serikali tunakwenda kufuta leseni zao wakitiwa hatiani na mahakama na kuwaweka kwenye orodha ambayo hawataruhusiwa kumiliki Leseni ya kufanya biashara yeyote katika mnyororo wa thamani wa madini Nchini Tanzania", amebainisha Mavunde.

Akielezea kuhusu  uchunguzi unaoendelea, Waziri Mavunde ameeleza kuwa,  watuhumiwa wamesema madini hayo ya dhahabu walikuwa wanasafirisha kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekea Visiwani vya  Zanzibar.

Mavunde amefafanua kuwa, kwasasa Uchunguzi na Mahojiano kwa  watuhumiwa unaendelea na pindi kazi hii ikikamilika tutawapandisha mahakamani ili kujibu mashtaka husika.

Sambamba na hapo, Waziri Mavunde amepongeza kazi nzuri  inayofanywa na Kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa madini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama 

Waziri Mavunde ametoa  rai kwa wafanyabiashara nchini kuacha tabia ya utoroshaji madini kwasababu  inarudisha nyuma juhudi za Serikali za  kukuza uchumi wa Nchi yetu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals