[Latest Updates]: Profesa Manya Aongoza Mdahalo Kuhusu Ushirikishwaji wa Wazawa Kwenye Utoaji wa Huduma (Local Content) katika Mkutano wa SADC

Tarehe : Aug. 8, 2019, 6:14 a.m.
left

Leo tarehe 08 Agosti, 2019 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya ameongoza mdahalo kuhusu ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye sekta mbalimbali nchini (local content) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mdahalo huo ulishirikisha pia Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe –Tawi la Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi na Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati kutoka Taasisi ya REPOA, Dk. Jamal Msami

Waliohudhuria katika mdahalo huo walikuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume ya Madini, Dk. Abdulrahman Mwanga, watendaji kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini pamoja na wadau kutoka taasisi za fedha na  wajasiriamali.

Awali akielezea manufaa ya ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye shughuli za madini na sekta nyingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa alisema kuwa ni pamoja na kuinua uchumi kuanzia katika ngazi ya chini na Taifa kwa ujumla.

Akielezea mafanikio ya utekelezaji wa mpango wa ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye shughuli zinazofanywa na wawekezaji nchini, Beng’l alisema wawekezaji kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo wameanza kutumia huduma zinazotolewa na watanzania hivyo kuongeza kipato.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ule wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, miundombinu, sekta ya madini na gesi.

Mapendekezo yaliyowasilishwa na wachangiaji mbalimbali kupitia mdahalo huo yalikuwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa watoaji huduma wa ndani kuhusu namna bora ya kutoa huduma na bidhaa bora, wazalishaji na watoa huduma wa ndani kuingia ubia na kampuni nyingine kubwa kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kupata uzoefu zaidi.

Akihitimisha mdahalo huo, Profesa Manya aliwataka wadau kutumia changamoto mbalimbali kwenye sekta mbalimbali kama fursa hususan kwenye utoaji wa huduma na kujipatia kipato.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals