Tarehe : Nov. 22, 2024, 6:55 p.m.
Ujumbe kutoka Burkina Faso umetembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kufanya Kikao kazi ili kujifunza kuhusu sekta ya madini,leo Novemba 22, 2024
Katika kikao kazi hicho
STAMICO imeeleza kwa kina namna serikali inavyoshiriki katika uvunaji wa rasilimali madini kwa kutoa wasilisho kuhusu inavyosimamia na kuendesha miradi yake ili kuhakikisha inaleta tija kwa Taifa
Akiongea kwa upande wa STAMICO Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mudrikati Kiobya amesema ili nchi iwezekunufaika na rasilimali madini ni vizuri Serikali kushiriki kwenye uchimbaji, kuwawezesha wachimbaji wadogo ili waweze kuendeleza rasilimali hizo.
Naye kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Burkina Faso Bw. HIEN Jonas, amesema wamefanya ziara ya kujifunza kuhusu STAMICO ili kuweza kutumia uzoefu huo kufanya uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwao.
Ameeleza kuwa nchini kwao hawana taasisi ya Serikali inayojihusisha na uvunaji wa rasilimali madini bali wana taasisi tofauti zinazowasimamia wachimbaji japokuwa wameanzisha taasisi ya serikali (Refinery )kwa ajili ya kununua na kusafisha dhahabu.
Ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kupitia STAMICO kwa maelezo mazuri yaliyoendana na matarajio yao kwani wameweza kujifunza jinsi ya kuwasaidia wachimbaji wadogo, sambamba na kuendesha miradi ikiwemo mradi wa kusafisha dhahabu na miradi mingine.
Utendaji bora wa STAMICO umeendelea kuwavuta mataifa mbalimbali kuja kujifunza namna Serikali inavyoweza kusimamia na kushiriki katika uvunaji wa rasilimali madini kwa manufaa ya taifa lake.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.