[Latest Updates]: Yaliyojiri Wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko Akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya Utekelezaji wa Vipaumbele vya Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 Bukombe Geita

Tarehe : July 12, 2022, 12:42 p.m.
left

#Katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya jumla ya shilingi 83,445,260,000.00 kwa ajili ya Wizara na Taasisi zake ili kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake.

#Bajeti hii ni sawa na ongezeko la asilimia 19.95 ya bajeti iliyopitishwa Mwaka wa Fedha 2021/22.

#Utekelezaji wa bajeti hii ya Mwaka wa Fedha 2022/23, utazingatia utekelezaji wa vipaumbele vya wizara kama tulivyopanga ambavyo vinalenga kuhakikisha rasilimali madini zinazidi kulinufaisha taifa letu kiuchumi na kimaendeleo kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya kitaifa

#Vipaumbele ambavyo Wizara imepanga kutekeleza Mwaka wa Fedha 2022/23 ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa; kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuwawezesha wananchi kushiriki uchumi wa madini.

#Vipaumbele vingine ni pamoja na kusimamia na kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya wizara na kuendeleza rasilimaliwatu na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.

#Utekelezaji wa vipaumbele hivyo utahusisha utekelezaji wa mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuanzisha na kusimamia migodi mikubwa na ya kati ya uchimbaji madini ya dhahabu na kinywe(graphite) na madini mengine na kuhakikisha migodi yote mikubwa, ya kati na midogo inaajiri watanzania

#Manufaa ya kufungua migodi hii ni kuongezeka mchango wa sekta katika Pato la Taifa, Uongezekaji wa ajira, na manufaa yatokanayo na uwajibikaji wa kampuni za madini kwa jamii (CSR) na ushiriki wa watanzania katika uuzaji wa bidhaa na utoaji huduma katika shughuli za madini.

#Mkakati mwingine ni kukusanya jumla ya shilingi bilioni 894.3 kiasi ambayo ni ongezeko la asilimia 22.12 ikilinganishwa na shilingi bilioni 696.4 zilizopangwa kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.

#Katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuwawezesha wananchi kushiriki katika uchumi wa Madini, wizara imepanga kuendelea kuwatengea maeneo au kuwapatia leseni kwenye maeneo ambayo yana taarifa za msingi za kijiolojia na kutoa huduma za utafiti kwa gharama nafuu.

#Katika mwaka wa fedha ujao, Wizara itaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji, uyeyushaji, usafishaji na utengenezaji wa bidhaa za madini; na kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani madini.

#Wizara itabuni na kutekeleza mikakati ya kuthaminisha uwekezaji katika Sekta ya Madini kwa kufanya tafiti za madini ya kimkakati, madini ya viwandani ya metali; kujenga imani kwa biashara ya madini nchini kwenye uwanja wa kimataifa.

#Niwakumbushe wadau wote wa Sekta ya Madini kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022. Katika Sensa itakayofanyika mwaka huu, itahusisha kipengele maalum kitachohusu masuala yanayohusu wachimbaji wadogo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Features Images
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals