[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yawasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge

Tarehe : Jan. 22, 2024, 8:25 p.m.
left

●Kuhusu mpango wa Serikali kununua dhahabu

●Kuhusu upatikanaji wa huduma kwa jamii inayozunguka mgodi.

●Ni kuhusu kupasuka kwa Bwawa la tope la Mgodi wa Mwadui.

Na.Samwel Mtuwa - Dodoma

Wizara ya Madini imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yaliyotokana na taarifa za shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa mwaka 2022 iliyowasilishwa Bungeni katika Mkutano wa Kumi wa Bunge.

Akiwasilisha taarifa hiyo leo Januari 22 , 2024 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini Augustino Ollal kwa niaba ya Waziri wa Madini amesema kulingana na maelezo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , mpango wa ununuzi wa dhahabu utetekelezwa kwa ushirikiano baina ya wachimbaji na wafanyabiashara ya dhahabu hapa nchini kwa watakaopenda kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania wataelekezwa kupeleka dhahabu yao kwenye viwanda vya kusafishia dhahabu vilivyoainishwa.

Ollal ameongeza kuwa mpaka sasa BoT imeweka lengo la kununua tani 6 za dhahabu zenye kiwango cha ubora wa kimataifa cha 99.99 kwa mwaka.

Akielezea kuhusu utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa huduma kwa jamii Ollal ameeleza kuwa wizara kupitia Tume ya Madini inaendelea kutoa mafunzo juu ya kanuni za kuchangia huduma kwa jamii zinazozunguka mgodi (CSR) kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa, viongozi wa migodi na watendaji wa Halmashauri ikiwemo halmashauri ya Msalala na Nyangh'wale.

Akiwasilisha kuhusu hatua zilizochukuliwa kutokana na tukio la kupasuka kwa bwawa la tope la mgodi wa Almasi wa Williamson , Ollal amesema baada ya uchunguzi kukamilika wizara ilisimamisha shughuli za mgodi na kuwataka kurekebisha sehemu zote zilizobainika na  mapungufu.

Ollal ameongeza kuwa kutokana utekelezaji wa hatua hizo mgodi umebadilisha msimamizi wa bwawa la tope ndani ya mgodi.

Hatua nyingine amesema wizara ya  madini itaendelea kuwasimamia wamiliki wa mabwawa ambapo mkakati maalum ni ufuatiliaji wa mabwawa yote nchini kufanyika kila wiki hususani kipindi chote cha mvua.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals