[Latest Updates]: Waziri Mavunde Akutana na Mwenyekiti wa Bodo ya EITI Jijini Dar es Salaam

Tarehe : April 4, 2024, 2:22 p.m.
left

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya kikao kifupi na Mwenyekiti wa Bodi ya EITI Rt. Helen Clark katika Ofisi Ndogo za Wizara  jijini Dar Es Salam.

Pia, kikao hicho kimehudhuriwa  na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI CPA Ludovick Utouh na Katibu Mtendaji wa TEITI Bi Mariam Mgaya pamoja na viongozi kutoka Wizarani.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mavunde amesema amefurahishwa na  ujio huo na kueleza kuwa ni wa kihistoria ikiwa ni ushirikishwaji wa Sekta ya Madini katika shughuli za Uwazi na Uwajibikaji.

Aidha, kikao hicho kimekubaliana kuwa Wizara ya Madini ikishirikiana na Asasi za Kimataifa ya EITI itatimiza kikamilifu mahitaji ya matakwa ya Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji katika shughuli mbalimbali za Usimamizi wa Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini. 

Pia, Mhe. Mavunde amesisitiza kwamba maoni yaliyotolewa katika ripoti ya Tathmani ( Validation Report ) kuhusu Uwazi na Uwajibikaji katika nchi ya Tanzania  iliyofanyika mwaka 2023 yatafanyiwa kazi kikamilifu.

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI CPA. Ludovick Utouh kwa niaba ya Katibu Mtendaji amesema dhana ya kuweka uwazi taarifa na takwimu mbalimbali za  Sekta ya Uziduaji ni kuhakikisha kuwa Rasilimali hizo zinawanufaisha wananchi na kuahidi kuwa  TEITI itatoa ushirikiano katika kutekeleza Matakwa hayo.

Ujumbe huo wa EITI ukiongozwa na Rt. Helen Clark utapata wasaa wa kukutana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Aprili 04, 2024.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals