[Latest Updates]: Msisafirishe Madini Ghafi nje ya nchi-Nyongo

Tarehe : Jan. 28, 2018, 10:36 a.m.
left

  • Ataka Wafanyabiashara kuwekeza Mirerani

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa agizo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kusafirisha nje madini yaliyoongezwa thamani badala ya madini ghafi ili kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017.

Nyongo aliyasema hayo Desemba 21, 2017, wakati wa Mnada wa Tatu wa Madini ya Tanzanite uliofanyika katika katika Kijiji cha Naisinyai, katika mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara na kushirikisha wafanyabiasha wa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia mnada huo, Nyongo alisema kuwa kwa sasa Serikali, inatekeleza Sera ya Viwanda katika kila sekta, hivyo kwa kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa katika Sekta ya Madini ni vyema madini yanayosafirishwa nje ya nchi yawe yameongezwa thamani kupitia viwanda vya hapa nyumbani.

Aidha, aliagiza kuwa Minada yote ya madini itakayofuata, iwe inauza Madini ya Tanzanite yaliyoongezwa thamani kwa kiwango kikubwa ili kutimiza matakwa ya sheria ya madini na kuunga mkono Sera ya Serikali ya uchumi wa viwanda.

 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza wakati wa Mnada wa Madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro.[/caption]

Vilevile, aliwahakikishia wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite kuwa serikali imeanza kutazama kero mbalimbali zinazoathiri ushindani katika kufanya biashara ya madini nchini kwa lengo la kuondoa kero hizo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wadau mbalimbali kuwekeza huduma muhimu katika Mji Mdogo wa Mirerani kwa kuwa mji huo kwa sasa ni kitovu cha biashara ya Madini ya Tanzanite .

Nyongo alisema kuwa, lengo la kuwekeza katika Mji Mdogo wa Mirerani ni kuwafanya wageni wanaofika katika mji huo wakati wa mnada kutumia fedha zao kwa kupata huduma mbalimbali na hivyo kuleta maendeleo zaidi kwa wakazi wanaozunguka mji huo.

“Napenda kutoa wito kwa wafanyabiashara na wadau wote nchini kuwekeza huduma muhimu katika Mji wa Mirerani kama vile Hoteli za kisasa, Taasisi za Fedha,Maduka ya kisasa na huduma nyinginezo ili wageni watakaofika hapa wasipate adha ya kutafuta  huduma hizo nje ya Mirerani badala yake fedha hizo zitumike hapa,” alisema Nyongo.

Alisisitiza kuwa huduma hizo zikiwepo zitachangia juhudi za Serikali katika kufungamanisha Sekta ya Madini na Sekta nyingine za Uchumi na kutafsiri suala la kunufaisha jamii katika eneo husika kiuchumi (Local Content) kwa vitendo.

Mnada wa Madini ya Tanzanite ulifanyika kwa muda siku tatu kuanzia Desemba 18-21 2017, ambapo kampuni 60 zilishiriki katika mnada huo kutoka nchi mbalimbali Duniani zikiwemo U.S.A, Sri Lanka, Hong Kong, India, China Thailand na wenyeji Tanzania.

Imeandaliwa na:

Zuena Msuya, Manyara

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals