[Latest Updates]: Wafanyabiashara wadogo wa madini Shinyanga kuuziwa asilimia tano ya almasi na mgodi wa WDL

Tarehe : Feb. 7, 2019, 9:03 a.m.
left

Waipongeza Serikali.

Na Greyson Mwase, Shinyanga

Wafanyabiashara wadogo wa madini ya almasi mkoani Shinyanga wanatarajia kuuziwa asilimia tano ya almasi inayochimbwa na Mgodi wa Almasi wa Williamson kama njia mojawapo ya kuwainua kiuchumi na kuimarisha masoko ya madini yaliyopo mkoani Shinyanga.

Akizungumza na wanahabari kutoka Idara ya Habari MAELEZO tarehe 06 Februari, 2020  kweye kituo kipya kilichoandaliwa kwa ajili ya kuuzia madini hayo mkoani Shinyanga,  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu alisimulia kuwa  kupitia mkutano wa wadau wa madini na Waziri wa Madini, Doto Biteko uliofanyika mapema Julai mwaka jana,  wafanyabiashara  wadogo wa madini waliomba kuuziwa asilimia tano ya madini ya almasi na Mgodi wa Williamson kama njia mojawapo ya kuimarisha biashara ya madini hayo na kujiongezea kipato huku Serikali ikipata kodi mbalimbali.

Alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ilifanya mawasiliano na Mgodi wa Williamson ambapo ilikubaliwa kuanza kwa mchakato ikiwa ni pamoja na ujenzi  wa kituo cha awali kitakachotumika kwa ajili ya kuuza madini husika kwa wafanyabiashara wadogo wa madini kwa njia ya mnada.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Kumburu alisema Serikali inaandaa utaratibu wa kugawa makinikia yaliyokuwa yanamilikuwa na Mgodi wa Williamson kwa wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kuyachenjua na kupata madini kwa ajili ya kuyauza.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wa madini katika mkoa wa Shinyanga, Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoani Shinyanga, Gregory Kibusi aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa hatua iliyochukua katika kuhakikisha wachimbaji wananufaika na rasilimali za madini.

Alifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini, wafanyabiashara wa madini mkoani Shinyanga wamekuwa wakiuza madini yao kwa uhuru na kulipa kodi mbalimbali Serikalini huku ulinzi ukiimarishwa kwenye masoko ya madini.

Katika hatua nyingine, Kibusi aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuacha utoroshaji wa madini na kuanza kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals