[Latest Updates]: Tume ya Madini Yatoa Bei Mpya Madini ya Vito

Tarehe : March 1, 2025, 2:06 p.m.
left

Kutumika kwa miezi mitatu

 TUME ya Madini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini, imekutana na wadau wa madini ikiwemo Wathaminishaji wa Madini, Wachimbaji Wadogo na Wanunuzi ili kupanga bei elekezi ya madini ya vito.

Akizungumza jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Venance Kasiki amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kufanya tathmini na kupanga bei mpya ya madini ya vito ambayo itatumika katika kipindi cha miezi mitatu na kuhakikisha biashara ya Vito inakwenda vizuri.

 “FEMATA ni mzalishaji wa madini, CHAMMATA  na TAMIDA ni wanunuzi wa madini ya vito, tumekutana ili kutengeneza bei elekezi, ambayo itatumika kwa kipindi cha miezi mitatu, ili pande zote ziweze kunufaika....; “Kikao kimeenda vizuri, bei zilizowekwa ni rafiki, zitanufaisha pande zote kwa maana ya wachimbaji, wanunuzi na serikali itapata stahiki zake ikiwemo Mrabaha na  Ada ya Ukaguzi,”amesema Kasiki na kuongeza

 “Bei zilizopendekezwa ni za wazi na zitapatikana kwenye mitandao na Tovuti ya Tume ya Madini, hivyo nawasihi wadau kupitia tovuti ya Tume ya Madini na ofisi za Afisa madini wakazi  ili kujua bei elekezi,”amesisitiza 


Aidha, Kasiki amesema pia wamebaini changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo wathaminishaji madini na kwamba watakuwa wanakutana nao kila robo ya mwaka lengo likiwa ni kutafuta suluhu ya changamoto hizo na kubadilishana uzoefu kutokana na mabadiliko ya teknolojia duniani katika tasnia ya uthaminishaji madini ili waende na wakati. 

Naye mwakilishi kutoka Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA) Kalebi Gunda akizungumza kuhusiana na bei elekezi amesema ni rafiki kwa wachimbaji.

“Kikao kimeenda vizuri hakuna atakayelalamika na kila mmoja atapata manufaa kwa upande wake, wachimbaji watanufaika, wanunuzi watanufaika na serikali nayo itapata stahiki yake ya mapaato kupitia Mrabaha na halmashauri itapata tozo yake ya ‘service levy’,”amesema Gunda

Vyama vilivyoshiriki kikao hicho ni Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA),  Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA)  na Chama cha Mabroka Tanzania (CHAMMATA)

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals