[Latest Updates]: Katibu Mkuu Samamba Akutana wa Ujumbe wa Marekani

Tarehe : July 16, 2024, 6:31 p.m.
left

Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba, ameupokea  ujumbe wa Serikali ya Marekani kupitia Ubalozi wake nchini  na kufanya kikao kifupi cha utambulisho ambapo ujumbe huo umeeleza kusudio la kufika Wizarani.

Akizungumza katika kikao hicho kifupi, kilichofanyika leo Julai 16, 2024, Mhandisi Samamba ameueleza ujumbe huo kuhusu mpango wa Wizara kuhuisha Mpango Mkakati wake ili kuiwezesha kukidhi matakwa ya  dhamira yake ya kuendeleza  madini muhimu na  mkakati  pamoja na utayari wa Wizara ya Madini kushirikiana na Marekani katika uendelezaji wa madini hayo na kuongeza  kwamba, Wizara Iko tayari kubadilishana taarifa za msingi zitakazowezesha kusudio la ushirikiano huo.

" Mkitoka hapa mtapata nafasi ya kukutana na taasisi zetu za GST, STAMICO na Tume ya Madini ambao watatoa mawasilisho yatayowasaidia ninyi kupata taarifa muhimu. Pia,  STAMICO  wanayo maeneo ambayo wangependa kushirikiana kuyaendeleza Kwa hivyo mtasikia mengi kutoka kwao," amesema Mhandisi Samamba.
 
Naye, Meneja  Mipango wa Idara ya Rasilimali Nishati na Madini  kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Bw. Evan McGlaughlin
amesema nchi hiyo imelenga kushirikiana na Tanzania katika maeneo kadhaa ikiwemo kuboresha mkakati wa kuendeleza madini mkakati, ushirikiano katika masuala ya jiosayansi na kuwajengea uwezo wataalam wa ndani.

Pia, ameishukuru Wizara kwa kuupokea ujumbe huo na kuukutanisha na taasisi zake utakaowezesha kuanzisha ushirikiano baada ya kuwa na majadiliano kwa takriban kipindi cha mwaka mmoja nyuma 

Itakumbukwa Tanzania inajiandaa vilivyo  katika  uendekezaji wa madini mkakati hususan kupitia Vision 2030: Madini ni Maisha& Utajiri katika kipindi hiki ambacho kuna mahitaji makubwa ya madini hayo duniani. 

Madini mkakati yanayotumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za teknolojia ikiwemo za betri za magari ya umeme, betri za simu na vizuia joto.

Madini hayo ni kama kinywe, nikeli, lithium, manganese, 
kolbati na mengine ambayo Tanzania imebarikiwa kuwa nayo.

#InvestInTanzaniaMiningSector

#Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals